SEHEMU
YA KUMI NA MBILI
Kweli sikutegemea kabisa macho yangu
hayakuweza tena kumuona mjomba, ni muda kidogo tu alikuwa ameshaaga na
kuondoka, pasipo hata matarajio yangu.
Taswira ya mama ndio ilinipokea baada ya kumuulizia
mjomba, kumbe muda mfupi tu alikuwa ameendoka. Sikutaka sana kujishughulisha na
habari zake, wakati huo akili yangu ilishaanza kukumbuka kuhusu kijitabu cha
kaka Eddy hivyo nilimuaga mama na kuingia ndani, kutokana na tabia nilikuwa
nimejizoesha muda wote wa kukaa ndani mama alishaizoe tabia ile hivyo, hata
aikumfanya uwenda kuhisi kitu ambacho muda wote kilikuwa kinanifanya niwe
ndani.
Nijitoma ndani, nikiwa na shauku kubwa sana,
taratibu niliwasha feni na kulifukuza joto katika namna iliyoleta faraja kwenye
mwili wangu huku nikiwasha taa kulifukuza giza ambalo lilianza kutaka kushamili
ndani ya chumba changu, kufanya macho yangu kuwa katika ubora wa hali ya juu.
Mikono yangu haikuchelewa kupambana kule nilipokuwa nimekiifadhi kijitabu kile.
Muda mchache macho yangu yalianza kupambana na maandishi yale, ambayo
yalionekana kunipa shauku ya kuliona jambo, muda ambao ulionekana si mrefu.
************
Kibao kilikuwa kimeendikwa maneno yalikuwa
yamesomeka closed yaani kumefungwa ndio yalipambwa nje ya mlango wa ofisi ile,
ambayo sikuwahi kutegemea uwenda kungekuwa kumefungwa kwa muda kama ule,
niliangalia saa yangu ilionesha vyema ilikuwa sasa tano kasoro, kwa muda kama
ule nilijua wazi uwenda hakuwa mbali muhusika wa ofisi ile ambaye ni mkuu wa
chuo kile.
Akili yangu haikuniupa kutoka eneo lile,
niliamua kujisogeza kidogo na kuketi kwenye moja ya viti vilivyokuwa nje ya
ofisi ile. Ambavyo havikuwa mbali sana na dirisha la ofisi ile. Wakati huo
sikujua kukaa kwangu eneo lile kungeleta dhahama kubwa sana kwa upande wangu, dhahama
ambayo sikuwahi kuitegemea uwenda ingenitokea katika siku ile ambayo ilikuwa ni
moja ya siku muhimu sana katika maisha yangu ya kuipata elimu kwa namna moja
ama nyingine.
Niliendelea kusubiri kwa muda kidogo kabla ya
ngoma za masikio yangu, kuanza kupitiwa na sauti ambazo hakika hazikuwa mara ya
kwanza kuzisikia, ni sauti hizo ambazo zilikuwa zinanifanya ni furahi kuwa na
mwanamke aitwaye Irene nikiwa ndani ya jambo ambalo wapenzi wote katika hii
dunia, wanalipa kipaumbele na kurifurahia kuliko mambo yote. Mwanzoni nilihisi uwenda masikio yangu
hayakuwa vyema kupokea sauti ile, lakini nilipojisogeza vizuri kwenye dirisha
lile sasa sikuwa na haja ya kubishana na sauti zile, ziliendelea kupenya vizuri
huku zikiuacha mwili wangu katika namna isiyoelezeka kibaya zaidi ni hata yale maneno
ambayo mara nyingi Irene alikuwa akipenda kuyatamka tukiwa kwenye zoezi hilo,
niliyasikia vizuri ya kimtoka huku sauti ya kugumia ya kumkuu wa chuo kile
ilikuwa ikitoka. Nilijiuliza mara mbili mbili huku nikiwa siamini ya kile
nilichokuwa nakisikia. Maswali mengi
yalijengeka kichwani mwangu kabla ya kunitoka neno la kizembe katika hali
ambayo hata mwenyewe ilikuwa ngumu kujisikia, ni hilo neno ambalo lilikuwa
likiomba eti asiwe Irene wangu, nilijitamani kujicheka lakini kicheko kilikuwa
mbali, na hata kingekuwa karibu na mimi hakika kingekuwa kicheko kilichojaa
uchungu ndani yake.
Uvumilivu ulinishinda nikiwa pale, niliamua
kujitoa mahali pale, kwa miadi ya kurudi kwa muda mwingine, sikutaka kuendelea
kusikiliza sauti zile, nilijitoa kinyonge kuliko hata nilivyokuwa nikitegemea.
Wakati huo kwa mbali kelele za wanafunzi ambao walikuwa uwanjani nilikuwa na
pambana nazo, sauti ambazo zilinikumbusha vicheko vya wale wasichana ambao
akili yangu sasa ilihusinisha na lile tukio, na kukiri uwenda walikuwa wanajua
maana ya vicheko vyao, ambavyo mwanzoni niliwatoa akili sasa nilijiona uwenda mimi
ndio nilikuwa sina akili. Japo niliampa kutojihusicha na msichana huyo lakini,
nguvu ya penzi ilikuwa ikininyanyasa.
Kweli ilininyanyasa katika kiwango cha juu
sana, miguu yangu ilitetemeka njia mule, nikipambana na ardhi ambayo niliona
muda si mrefu ilikuwa inataka kunidhalilisha, katika namna ambayo sikuwahi
kuitegemea, na hata nilipojikaza bado nilishindwa. Niliamua kujitoma ndani ya
darasa moja ambalo lilionekana liko wazi, taratibu niliamua kuketi kwenye moja
ya kiti ambacho kilikuwa kimejitomea kimeza kidogo mbele yake. Ambacho kiliupa
hifadhi mwili wangu punde nilipojiweka kwenye kiti, baada ya kukisogeza karibu
nami, nilijiinamia chini kwa muda kidogo lakini hatimaye fikra zangu zikasiliti
kile kiti huku ikijenga taswira ya mkuu yule wa chuo, na Irene wangu.
Kabla ya kupingana na kile nilichokuwa na
kisikia kwenye dirisha la ofisi ile, ya kuwa hakuwa Irene wangu, roho ya
kupingana na lile ilianza kunitawala huku nikitamani kwenda kuhakisha juu ya
lile. Ukweli ilinisumbua niliamua kujitoa haraka.
Ajabu sasa, bora ningeiamua kubaki kule kule,
nisingehitaji ushahidi wa kile. Masikio
yangu yangetosha kuwa shahidi kabisa.
Maana macho yangu sasa yalikumbana na dhahama ile, ni kweli alikuwa
Irene. Macho yangu yaliendelea kupambana na mwanamke yule punde alipokuwa
akijitoa kwenye ofisi ile ya mkuu wa chuo, utadhani hakuna kilichokuwa
kinaendelea ndani yake. Nikiwa nimesima kwa mbali kidogo lakini umbali ambalo
ulikuwa ukiniwezesha vyema kuona vizuri kile kilichokuwa mbele yangu, na uzuri,
Irine hakuwa mgeni kwangu.
Nguvu ziliniishi na hata hamu ya kuendelea
kubaki ndani ya chuo kile haikuwepo kabisa, miguu yangu ilishaanza kugeuza njia
ya kurejea nyumbani huku akili yangu ikiwa nzito kuliko kawaida, mwili
ukiendelea kupambana na maumivu ambayo hayakuwa ya mchezo hata kidogo. Mawazo
mengi yakiwa yanakikabili kichwa changu nikiwa ndani ya daladala nikirejea
nyumbani. Alimanusura nipitilizwe sehemu ya kituo cha nilipokuwa na shuka.
Hali yangu haikuwa sawa hata niliporejea
nyumbani, siku nzima kwangu ilikuwa mbaya, ijapokuwa nilijitahidi kuificha sana
mbele ya mama ambaye kwa upande wake siku hiyo alionekana kama anajambo ngumu
linamkabiri hivyo hakujihusisha sana na mimi na hata mdogo wangu Criss siku hiyo
si kumkuta nyumbani, alikuwa amekuja kuchukuliwa na mjomba, ambaye nilipata taarifa zake punde
nilipoona kuna tofauti kidogo ambayo hapo awali haikuwepo pale nilipoamua
kumuliza mama ambaye alikuwa akiendelea kujishughulisha japo kiuvivu uvivu, ni
kama alikuwa anajua uwenda jambo zito lilikuwa linakwenda kutokea katika
familia yetu, ni kweli ni kama alikuwa anajua lakini alikuwa tayari amechelewa.
Roho yangu haikuwepo tena dunia, kwa muda ule, maana nilipojitoma ndani,
sikuona faida ya kuishi katika dunia. Dunia ambayo katika jicho la kawaida
niliona hainitaki kabisa, Kiukweli niliamua kufanya maaumuzi haya, huku
nikimsihi Mungu.
Post a Comment