Rais wa Zimbabwe
Robert Mugabe amepuuzilia mbali taarifa za hivi karibu za uvumi juu ya
afya yake, kwa kutoa mzaha kwamba alikufa na akafufuka.
Akionekana
mwenye furaha, Mugabe mwenye umri wa 92, aliyasema hayo alipokuwa
akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Harare akitokea nje ya nchi.
Taarifa ya safari yake ilisema kuwa ndege yake ilikuwa ikielekea mashariki mwa Asia, na kwamba badala yake ilikwenda Dubai.
Bw Mugabe alisema kuwa alikwenda huko kwa masuala ya kifamilia.
Mnamo mwezi Mei, Mke wa Mugabe, Grace, alisema kuwa mumewe ataongoza nchi hata akiwa kaburini.
Taarifa
za uvumi kuhusu safari zake za ndege na nyinginezo, zilisababisha
kuenea kwa tetesi kwamba afya ya Bw Mugabe ilikuwa mbaya na kwamba
alikwenda Dubai kwa matibabu ama hata alikuwa tayari amepoteza maisha.
Tovuti
ya Gazeti linalochapishwa kila siku la Southern Daily, ilituma makala
yenye kichwa cha habari "Robert Mugabe anauwa kiharusi, Mnangagwa sasa
ndie rais wa mpito wa Zimbabwe".
Emmerson Mnangagwa ni makamu rais wa Zimbabwe.
Post a Comment