September
Mosi 2016 Rais Magufuli amezungumza katika mkutano wa 14 wa mwaka wa
wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es
salaam.
Katika
kile kinachoonekana ni kutaka kuwadhibiti watu wanaodaiwa kuficha fedha,
Rais Magufuli amesema kuwa mamlaka aliyonayo anaweza kuamua kubadili
fedha ili zile zinazofichwa na watu hao wakose mahali pa kuzipeleka.
Aidha
amesisitiza kuwa katika utawala wake fedha za bure hazitakuwepo kwa
sababu zilikuwepo awali zilitokana na fedha za wizi kutoka serikalini
ambazo kwa sasa zimedhibitwa, alisema kwa mwendo anaokwenda nao sasa
sasa ni ngumu kwa mwananchi kupata fedha bila kufanya kazi
SOURCE: MWANANCHI
Post a Comment