0

Baada ya Simba kuituliza Azam kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, leo wametepeta tena mbele ya Ndanda FC ya Mtwara kwa magoli 2-1.

Azam imepoteza game ya pili mfululizo kwenye ligi ikiwa nje ya uwanja wao wa Azam Complex. Ndanda baada haijapoteza mechi kwenye uwanja wake wa Nyumbani tangu kuanza kwa ligi.

Magoli ya Ndanda yamefungwa na Omary Mponda na Raphat Hamisi huku John Bocco akiifungia Azam goli pekee.

Matokeo hayo yanaendelea kuifanya Azam ibaki na pointi 10 ikiwa imeshacheza game 6 na kuipa nafasi Simba kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi 3.

Matokeo mengine:

Mtibwa Sugar 1-1 Mbao FC

Tanzania Prisons 0-0 Mwadui FC

Ruvu JKT 2-0 Mbeya City

Post a Comment

 
Top