0


Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Magdalena Sakaya amesema amewasilisha barua ya rufaa katika mkutano mkuu wa chama hicho kupinga kusimamishwa uanachama. 
Dodoma. Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Magdalena Sakaya amesema amewasilisha barua ya rufaa katika mkutano mkuu wa chama hicho kupinga kusimamishwa uanachama.

Hivi karibuni, Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho lililoketi visiwani Zanzibar lilimsimamisha uanachama Sakaya kutokana na kile kilichoelezwa ni kuvunja katiba kwa  kutohudhuria kikao bila kutoa taaarifa.

Akizungumza na nje ya Ukumbi wa Bunge Dodoma , Sakaya ambaye ni mbunge wa Kaliua amesema: “Pia, nimemwandikia barua Spika wa Bunge, Job Ndugai na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi  kuwaelezea kuwa sikubaliani na uamuzi wa baraza hilo kwa kuwa ni batili,” alisisitiza.

Mbali na Sakaya, wengine waliosimamishwa ni aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, Abdul Kambaya, Ashura Mustafa, Omar Mhina na Thomas Malima.

Wengine ni Kapasha Kapasha, Maftaha Nashuma, Mohammed Mnyaa, Haroub Shamis na Mussa Haji Kombo huku wajumbe wawili wa baraza hilo, Rukia Kassim Ahmed na Athuman Henku wakipewa onyo.

Post a Comment

 
Top