Mkuu wa mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi akizungumza na wanachi wa wilaya ya Liwale
Mkuu wa mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi amewata wananchi wa
wilaya ya Liwale mkoani Lindi kuitunza mikorosho ili kuongeza mavuno na kuuza
mazao yao ya korosho kwenye vyama vya misingi vya mazao na amewashauri wakulima
kuweza kufungua akaunti kwenye banki ili mazao yao yakiuzwa waweze kupokelea
pesa kwa njia banki.
Mkuu wa mkoa huyo aliyasema hayo leo akizungumza na wananchi
kwenye mkutano wa hadhala uliofanyika kwenye viwanja vya Nanjinji katika kata
ya Likongowele wilayani hapa.
Godfrey Zambi amewaonya watumisha wa serikali wasijihusishe na
ulangazi wa ununuzi wa kangomba na watumishi watakaopatikana na ulangozi huo
watapoteza kazi zao na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao, watumishi
wanaotaka kujihusisha na ununuzi wa korosho waende kwenye mnada wakanunue.
Bwana zambi aliwaomba wanaliwale kuendeleza kudumisha amani
ya Taifa na kuepuka tabia ya kubaguana amewataka wananchi kushirikiana kwa
pamoja ili kuweza kujenga taifa pia amekemea wanasiasa wanatoka mkoa ungine kuja
kufanya siasa Liwale kitendo hicho hakiwezi kutatua kero za wanananchi hao bali
amewataka viongozi wa eneo husika kufanya mikutano kwa wananchi wao na kuweza kuchukua kero na
kuweza kuzitatua.
“Wakati wa kampeni wakati wa wanasiasa kunadi sera zao uchaguzi
ukishafanyika tunaamisha siasi zetu
bungeni au kwenye mabaraza ya madiwani hatuwezi kulumbana kwenye maeneo ya
maendeleo muda wote wale waliochaguliwa waende kwenye mabaraza wakalumbani huko
lakini wakazungumze mambo ya maendeleo huko” alisema Zambi
Aliongeza kwa kusema viongozi wa jimbo la Liwale wafanye
mikutano kwenye maeneo yao na ndio wanaojua kero za wananchi kuliko viongozi
wanaotoka nje ya mkoa husika kuja kufanya siasa kwenye mkoa uingine.
Godfrey Zambi aliwakumbusha wananchi juu ya suala la janga la
ugonjwa wa Ukimwi amewataka wananchi kuwa waaminifu kwenye mahusiano yao za
ndoa kama watashindwa kuwa waaminifu watumie kinga na amewataka wananchi
wasiwanyanyapae wale wanaoishi na
ugonjwa wa Ukimwi.
Katika mkutano huo baadhi ya wananchi waliweza kupata nafasi
ya kutoa kero zao kama Rafii Likochelo alisema moja ya kero yake anaidai ofisi
ya ardhi fidia ya shamba lake kiasi cha shilingi milioni moja na laki tatu na
elfu hamisi (Milioni 4,350,000/=) alidai deni hilo ni la muda mrefu licha ya
kwenda mkoani na kupewa barau mpaka sasa hajaweza kupata fidia hiyo.
Nae Idaya Chikawe alimuomba mkuu wa mkoa kumaliza mgogoro
uliopo wa mipaka uliopo katika kijiji cha Kikulyungu katika mgogoro huo umeweza
kusababisha madhara mbalimbali ikiwemo kutopotea kwa watu na kusabisha wanawake
kupoteza wanaume wao.
Godfrey Zambi aliweza kutoa majibu juu ya kero hizo alisema
suala la mgogoro wa mpaka katika kijiji cha Kikulyungu ataushughulikia ndani ya
miezi 3 utakuwa umeisha na jana (septemba 5) alielekea kijijini huko na
kuzungumza na wananchi na suala la fidia la Likochelo amemuagiza mkuu wa wilaya
Sarah Chiwamba kukaa na viongozi wa ardhi na kuweza kutatua kero hilo.
Post a Comment