0

Katika dunia ya leo, ambayo ipo kwenye ushindani mkubwa ili uweze kufanikiwa unalazimika kujifunza mambo mengi ya kukusaidia kufanikiwa huko. Bila kufanya hivyo hautaweza kufanikiwa na kufikia viwango vya juu, zaidi utaishia kuwa na mafanikio ya kawaida kabisa.

Haijalishi uwe umeajiriwa au umejiajiri ni muhimu kujua mambo mengine ya ziada ambayo tena ni ya kawaida lakini, yanaendana na kasi ya ulimwengu wa sasa. Kwa jinsi utakavyojua mambo hayo utazidi kujiongezea thamani kubwa ambayo bila ubishi itazidi kukupa mafanikio.
Yafuatayo Ni Mambo 10 Ambayo Ni Muhimu Kuyafahamu Kwenye Maisha Yako.

1. Kuongeza maarifa.
Kila siku na kila wakati, jenga tabia ya kuongeza maarifa. Jifunze kupitia vitabu au semina mbalimbali. Kuunoa ubongo inatakiwa iwe sehemu ya maisha yako na  ni hatua muhimu sana ya kukusaidia kufikia mafanikio makubwa kuliko unavyoweza kuwaza au kufikiri. Watu wenye mafanikio wanajifunza sana kila siku.

Ongeza maarifa yako kila siku.

2. Kutengeneza bajeti.
Huhitaji kusomea uchumi ndio uweze kupanga bajeti. Katika maisha yako pia unahitaji kujifunza juu ya upangaji wa bajeti zako binafsi. Hiyo itakusidia kutokuwa na matumizi ya hovyo ya pesa zako. Pia bajeti itakusaidia kutunza pesa na kukusaidia kuwekeza kwa siku za baadae.

3. Kuwasikiliza wengine vizuri.
Ni vyema kujua namna ya kuwasikiliza wengine vizuri. Acha kuwa muongeaji tu kila wakati na kusahau kuwasikiliza wengine. Unapowasikiliza wengine inakusaidia kujifunza mambo ya msingi ambayo ingekuwa sio rahisi kwako kujifunza kama ungekuwa unaongea wewe tu.

4. Kongea mbele ya watu wengine.
Jambo lingine ambalo hutakiwi kukwepa kujifunza ni kuongea mbele za watu. Lazima uwe na maarifa ya kukusaidia kuogea mbele za watu. Ikiwa utakuwa unaogopa kuongea mbele za watu jiulize, ni nini kitatokea ikiwa utapewa jukumu hilo? Hivyo unalazimika kujifunza hili pia kwa faida yako.

5. Kujifunza lugha zingine.
Kwa dunia ya sasa jinsi ilivyo, si ya kukaa na kujivunia lugha ya aina moja. Ni vizuri ukawa na tabia ya kujifunza lugha nyingine za kigeni angalau hata moja pole pole. Hiyo itakusaidia hasa pale unapotaka kujifunza kitu kwa mfano kupitia vitabu haitakuwa tabu sana kwako kwa sababu lugha utakuwa unaijua.

6. Kuwa na mwonekano mzuri.
Moja ya kitu kizuri cha kukusaidia kukutambulisha ni mwonekano mzuri ulionao. Unapokuwa na mwonekanao mzuri inakusaidia kukutambulisha wewe ni nani. Pia Mwonekano wako unakuwa unakutangaza kwamba wewe ni mtu wa aina gani katika jamii husika.

7. Kulinda siri za wengine.
Ni vyema katika maisha ukajifunza pia kuwa mtu wa kutambua na kulinda siri za watu wengine. Usiwe mwongeaji sana wa mambo yasiyo kuhusu hasa ya watu wengine. Linapotokea jambo ambalo unaona linaweza likawa siri, ni vyema kukaa kimya kuliko ukawa mvujishaji wa mambo ya watu.

8. Kutumia kompyuta kwa ufasaha.
Haijalishi wewe ni bosi au muajiriwa. Ni muhimu sana kujifunza juu ya matumizi ya kompyuta. Hapa unatakiwa ujue program mbalimbali kama ‘Microsoft office au Excel’ ambazo zinaweza kukusaidaia. Pia kwa kujua kompyuta hata ikitokea umepata kazi sehemu, zipo ofisi ambazo hazihitaji sana secretary maarifa hayo yatakusaidia.

9. Kuendesha gari.
Unaweza ukaona ni kitu cha kawaida lakini lazima ujue kuendesha gari. Hii sio dunia ya kusubiri eti ununue gari ndio ujue kuendesha. Ni muhimu kujifunza kuendesha gari na hiyo itakusaidia kukuongezea wasifu kwenye mambo mengine kama ya kazi au kukupa uzoefu binafsi hata wewe.

10. Kupika.
Si vibaya ukawa na maarifa ya kupika pia. Haijalishi wewe ni mwanume au mwanamke ni muhimu kujua kupika hata kidogo. Jiulize kama hutaki kabisa kupika wale wanaokupikia siku wasipofanya hivyo utafanyaje? Naamini itakusumbua na itakuwa shida kwako. Hivyo ni muhimu kujua kupika na hilo jukumu lisibaki kwa wanawake tu hata kwa wanaume pia.

Hayo ni baadhi tu ya mambo machache ambayo unalazimika kuyafahamu katika maisha na mafanikio yako kwa ujumla. Unaweza ukajifunza mambo mengine zaidi kwa kadri unavyoweza.

Post a Comment

 
Top