0


 Mbunge wa jimbo la Liwale,Mheshimiwa Zuberi Kuchauka akikagua ujenzi wa daraja septemba 27 katika kijiji cha Kimambi wilayani Liwale.

Ujenzi wa daraja umeanza rasmi katika kijiji cha Kimambi wilaya ya Liwale mkoani Lndi lililobomolewa na maji ya masika katika barabara ya Nangurukuru kwenda Liwale.

Mbunge wa jimbo la Liwale,mheshimiwa Zuberi Kuchauka ametembelea katika daraja hilo na kuona ujenzi ukiendelea vizuri ili kuweza kurejesha mawasiliano katika wilaya hiyo ya Liwale.

 "Nashukuru ujenzi umeanza pia namshukurani meneja wa Tanroad mkoa wa lindi, Juhudi zako za kuturejeshea mawasiliano ya barabara wana Liwale zinaonekana na tuendelee kushirikiana" alisema Mheshimiwa Kuchauka

Post a Comment

 
Top