Mkuu
wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi akikagua paredi ya vijana 1140
wa operesheni Magufuli kwa mujibu wa sheria katika kikosi cha 825 KJ
kilichopo Mtabila katika Wilaya ya Kasulu, Mkoani Kigoma.
Na Abel Daud, Globu ya Jamii, Kigoma
Mkuu
wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi amewataka vijana waliohitimu
mafunzo ya operesheni Magufuli (kwa mujibu wa sheria) kutoka wilayani
hapo kwenda kutekeleza falsafa ya hapa kazi tu.
Hayo
ameyasema alipokuwa akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana
1140 operesheni Magufuli kwa mujibu wa sheria katika kikosi cha 825 KJ
kilichopo Mtabila katika Wilaya ya Kasulu na kuwataka kwenda kuungana na
watanzania wengine wote katika kuiamini kuitekeleza na kuiishi falsafa
ya hapa kazi tu kwa vitendo.
Akisoma
taarifa fupi kwa mgeni rasmi, Mkuu wa kambi ya 825 KJ, Meja George
Kazaula amesema kikosi kimefanikiwa kutengeneza madawati 1074 ikiwa ni
agizo la Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.
John Magufuli.
Pia
ameelezea changamoto zinazoikabili kambi hiyo kuwa ni pamoja na
kukosekana kwa umeme wa gridi ya taifa pamoja na miundombinu ya barabara
kuwa mibovu hali inayopelekea matumizi makubwa ya uendeshaji wa umeme
wa genereta pamoja na matengenezo ya mara kwa mara ya magari ya kikosi.
Nae
mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga taifa hapa nchini Luten col.
Philipo Mahende amewataka vijana hao kuwa wazalendo wa kweli ambao
watakuwa tayari kulilinda taifa kwa gharama yoyote ile ili amani,umoja
na mshikamano miongoni mwa watanzania unakuwa endelevu, na kuwaomba
kujiepusha na kutokuwa miongoni mwa watanzania wachache wanaoshabikia
mgawanyiko miongoni mwetu kwa misingi ya itikadi za kisiasa,kidini au
mahali anapotoka mtu.
Akisoma
lisara kwa mgeni rasmi mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo ameiomba
serikali kuiongeza bajeti Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa ili
vijana wengi wapate nafasi kujiunga na mafunzo ya JKT ili waweze
kujifunza uzalendo na shughuli za uzalishaji mali ili kuwatengenezea
uwezo wa kujiajiri wenyewe pasipo kuitegemea Serikali.
Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi akitoa zawadi kwa baadhi ya vijana waliofanya vizuri katika mafunzo hayo
Vijana hao Wakipita kwa mwendo wa haraka.
Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi akipokea heshema ya kijeshi kutoka kwa vijana wanaohitimu
Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi wa kwanza kushoto akielekea yalipo madawati.
Baadhi ya madawati yaliyotegenezwa.
Baadhi ya vijana wa JKT Mtabila wakiendelea na kazi ya kupaka rangi madawati.
Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi akiangalia madawati yaliyotegenezwa kambini hapo.
Vijana wanaomaliza mafunzo ya opeteshen Magufuli wakipita kwa mwendo wa kasi mbele ya mgeni rasmi.
Meja George Kazaula akisoma taarifa fupi
Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi akitoa hotuba
Post a Comment