Mtu wangu
taarifa inayogonga vichwa vya habari kwa sasa kwenye vyombo vya habari
vya kimataifa ni hii ya Mfalme wa Japan kuonyesha nia ya kutaka kuondoka
madarakani wakati katika sheria za nchi hiyo hakuna nafasi inayomruhusu
mfalme kuondoka madarakani.
Mfalme wa
Japan Akihito amelihutubia taifa hilo kupitia runinga ambapo ameeleza
kuwa ametaka kung’atuka kutokana na kwamba ana wasiwasi na umri na
udhoofu wa afya yake huenda vikamfanya ashindwe kutekeleza majukumu
yake.
Wananchi wa Japan wakifuatilia hotuba ya mfalme
Lakini
muda mfupi baada ya hotuba yake, Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe,
amesema atatathmini kwa makini nia hiyo ya mfalme huyo. Mfalme Akihito
amekuwa madarakani tangu kifo cha babake, Hirohito, mwaka 1989, habari
kwamba anataka kung’atuka zilianza kutokea kwenye vyombo vya habari
mwezi jana.
Wananchi wakionekana kushangaa baada ya Mfalme Akihito kutangaza nia yake ya kung’atuka
Post a Comment