Vikao
vya bunge la 11 limeendelea tena leo bungeni Dodoma September 13 2016
ambapo katika kipindi cha maswali na majibu Naibu Waziri wa mambo ya
ndani ya nchi Mwigulu Nchemba ametoa ufafanuzi wa swali la mbunge wa
viti maalum CHADEMA Susan Maselle aliyehoji hatua za serikali kuhusu
baadhi ya wanajeshi kuwabambikia kesi wananchi.
Waziri Nchemba amesema…>>>’Jeshi
la Polisi linafanya kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni, miongozo na
taratibu. Wale wanaobainika kukiuka maadili ya jeshi huchukuliwa hatua
kwa kuwapa adhabu mbalimbali ikiwemo kuwafukuza kazi‘
‘Mtu
yeyote anayeona kuwa anaonewa anapaswa kuwasilisha malalamiko yake
katika vyombo vya kisheria pindi anapoona hatendewi haki kutoka kwa
Polisi kwa mujibu wa sheria za nchi‘ –Waziri Nchemba
Kuhusu tuhuma za Polisi kuwakamata wanasiasa na viongozi wa dini kisha kuwaweka rumande kwa muda mrefu? Waziri Nchemba kasema…>>>’Jeshi la Polisi halikamati watu kwa itikadi ya dini zao bali huwakamata kulingana na makosa yao na kuwafikisha mahakamani‘
Post a Comment