0

Missenyi . Wakazi wawili wa  Mtukula wilaya ya Missenyi mkoani Kagera wamepoteza maisha baada ya kupigwa na radi kufuatia  mvua iliyonyesha jana kuanzia  majira  ya  saa  sita  mchana.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Agustine Ollomi aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Amis Abdul anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 40 hadi 50 na Shafi Saidi miaka  30 hadi 35 wote wakazi wa Mtukula wilayani Missenyi.

Mvua hiyo ilionyesha kwa takribani dakika 35 ikiwa imeambata na upepo ambapo watu hao wamepigwa na radi wakiwa wanaendelea na shughuli zao za kuchinja  katika maandalizi ya kusherekea Eid El Hajj.

Post a Comment

 
Top