August 29 2016 Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye alitangaza kuvifungia vituo viwili vya radio kwa muda usiojulikana ambavyo ni Magic Fm ya Dar es salaam na Radio 5 ya Arusha kwa makosa ya kutangaza na kutoa habari za kichochezi.
Waziri Nape alielekeza kamati ya maudhui kuviita vyombo hivyo na kuwasikiliza kwa kina kisha kushauri hatua zaidi ya kuchukua.
Leo
September 16 2017 kamati imetoa maamuzi ambapo Magic FM wamepewa onyo
kali na kutakiwa kuomba radhi kwa siku tatu mfululizo kuanzia kesho
September 17 2016, Redio 5 imepewa adhabu ya kulipa shilingi milioni 5,
kufungiwa miezi 3 na kuwekwa chini ya uangalizi wa mwaka mmoja.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.