0
 Mchezaji wa Sido fc mwenye jezi nyekundu akiumiliki mpira kwenye mchezo wa jana dhidi ya timu ya Kitogoro fc mchezo uliopigwa uwanja wa wilaya ya Liwale





 Mchezaji wa timu ya Sido fc Haikosi Mpwate akiwa chini mara baada ya kuchezewa lafu na mchezaji wa timu ya Kitogoro fc

Ligi ya Alizeti cup hatua ya nusu fainali jana septemba 6 imeweza kumalizika kwa kupigwa mchezo mmoja kati ya Sido fc dhidi ya Kitogoro fc katika uwanja ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Katika mchezo huo timu ya Sido fc iliweza kuibuka na ushindi wa magoli 2 kwa bila huku goli la kwanza Sido fc likifungwa na Kibiga Kibiga katika dakika ya 19 goli lilodumu mpaka mapumziko ya dakika 45.

Katika kipindi cha pili Kocha wa timu ya Kitogoro fc,Abdelehemani Ndwimbwage aliweza kufanya hisabu za kubadilisha wachezaji lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda baadae alizidiwa  mbinu za kimchezo na kocha wa Sido fc, Mohamedi Hema, kuweza timu ya Sido fc ikiongeza goli la pili katika dakika ya 69 lililofungwa na Saidi Mohamedi mpaka dakika 90 zinakamilika Sido fc waliweza kuibuka na ushindi wa magoli 2-0.

Septemba 5 kulikuwa na mchezo wa hatua ya nusu fainali kati ya timu ya Hawili dhidi ya New Boys mchezo uliotimua vumbi katika uwanja wa wilayani hapa na Hawili fc waliibuka na ushindi wa magoli 9-0 katika kipindi cha kwanza timu ya Hawili iliweza kuongoza magoli 5-0.

Katika kipindi cha pili timu ya Hawili fc iliweza kuongeza magoli 4,magoli ya Hawili fc yalifungwa na Faraja Hasani katika dakika ya 10,24 na 41,Imani Mbesigwa dakika ya 37,Faustin Ibrahim dakika ya 45,57 na dakika 80 na magoli mawili yakifungwa na Ramadhani Hashimu kaika dakika ya 71 na dakika ya 89.

Kwa mujibu wa mratibu wa mashindano,Selemani Nangomwa alisema hatua ya mchezo wa kumpata mshindi wa tatu mchezo utapigwa septemba 8 kati ya timu ya New Boys dhidi ya Kitogoro fc katika uwanja wa wilayani hapa.

Mchezo wa fainali utatimua vumbi septemba 9 kati ya timu ya Hawili fc dhidi ya watani wao wa jadi Sido fc mchezo unatarajiwa kuwa na mashabiki wengi na utaweka rekodi mpya ya kuwa na watazamaji wengi zaidi kutokana na timu hizo kuwa na mashabiki wengi sana kutoka kila viunga vya wilayani.

Baadhi ya wadau wa soka wakizungumza na Liwale Blog walishauri siku ya mchezo wa fainali kati ya Hawili fc dhidi ya Sido fc kuimalishwe ulinzi kwakuwa mashabiki watakuwa wengi sana wakiongeza baadhi ya mashabiki hupenda kukaa maeneo ya golini na kumsemesha golikipa.

Zawadi zimetajwa zitakazotolewa kwa washindi mbalimbali mshindi wa kwanza atapewa pesa taslimu shilingi laki tano (500,000) pamoja na kombe lenye thamani ya shilingi laki tatu na elfu hamsini (350,000) pamoja na jenzi,nafasi ya pili atapewa shilingi laki mbili na elfu hamsini (250,000) pamoja na jenzi na nafasi ya tatu atapata shilingi laki moja na elfu hamsini (150,000) pamoja na jenzi.

Zawadi zingine zitatolewa kwa mchezaji bora,mfungaji bora,golikipa bora,kocha bora na mwamuzi bora kila mmoja katika nafasi hii atajinyakulia shilingi elfu ishirini (20,000).

Ligi hii ni maalum kwa kuhamasisha wakulima wa wilayani hapa,walime zao jipya la Alizeti ambalo ni maarufu kwa mikoa ya Dodoma,Singida na Shinyanga.

Post a Comment

 
Top