Mkuu wa wilaya Lindi Shaibu Ndemanga,ametoa
onyo kwa viongozi wa dini na wazazi walio na tabia ya kuoa na kuozesha
mabinti walio na umri mdogo,wakiwemo wanafunzi kuacha mara moja mpango
huo,vinginevyo Sheria itachukuwa mkondo wake,ikiwemo kuwakamata na
kuwafikisha Mahakamani.
Ndemanga
ametoa onyo hilo jana, wakati anazungumza na watumishi wa Idara
mbalimbali wa Serikali na viongozi wa dini,waliopo wilayani humo,katika
kikao kazi kilichofanyika kata ya Mtama,na kufanyika ukumbi wa kituo cha
maendeleo ya jamii,kijiji cha Mtama.
Ndemanga amelazimika kutoa onyo hilo
kutokana na kile kinachoelezwa wapo baadhi ya viongozi wa
dini,wakishirikiana na wazazi kufungisha ndoa mabinti walio na umri
mdogo wakiwemo wanafunzi wakikatishwa masomo yao,kisha kuozeshwa kwa
tama ya kupata fedha za mahali.
Aidha,kiongozi
huyo wa wilaya ya Lindi,amesema mzazi au kiongozi yeyote wa dini
atakayebainika kufungisha ndoa mwanafunzi anayesoma wa Shule za msingi
na Sekondari,watakamatwa na kufikishwa Mahakamani.
Pia,amewaagiza watendaji wa vijiji na
kata kwenye maeneo yao, kuhakikisha wanaorodhesha majina ya wazazi na
walezi walio na tabia ya kuwakatisha masomo wanafunzi wa kike,na kuwaoza
kwa ajili ya tama ya fedha.
Post a Comment