Mkuu
wa Chama cha Wafugaji Tanzania (pichani kati),Magembe Makoye akizungumza
mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar
kuhusiana na mambo mbalimbali yanayowakabili wafugaji hapa
nchini,kushoto ni Mfugaji kutoka Suwambawaga,Mayunga Gamas na kulia ni
Charles Mtokambati.
Bwa.Maghembe
Makoye alieleza changamoto mbalimbali zinazowakabili wafugaji hao kuwa
ni Ukosefu wa Maeneo rasmi ya malisho,Migogoro Baina ya Wakulima na
Wafugaji,Migogoro kati ya Wafugaji na Idara ya Maliasili na
Wanyamapori.Akaeleza kuwa kwa sasa kuna Mgogoro mkubwa kati ya Idara za
Maliasili na Wanyamapori ndani ya Wizara ya maliasili na utalii na
Wafugaji,akafafanua kuwa changamoto hizo zimekuwa sugu kutokana na
kupanuka kwa maeneo ya Maliasili na kuchukua maeneo ya Wafugaji.
"Wafugaji
wamekua wakifukuzwa kutoka kwenye maeneo hayo ambayo hapo awali
walikuwa wakiyatumia kwa malisho,baada ya kuchukuliwa na maliasili na
kuwa sehemu ya maeneo yaliyohifadhiwa.
Mkuu
wa Chama cha Wafugaji Tanzania (pichani kati),Magembe Makoye akionesha
baadhi ya Nyaraka kwa waandishi wa habari,zinazoeleza kukamatwa kwa
ng'ombe za wafugaji hao zaidi ya elfu moja na Wizara ya Maliasili na
Utalii,ambapo mahakama iliamua kuwa Maliasili na Utalii irejeshe Ng'ombe
hao kwa wafugaji,ambapo mpaka sasa kwa mujibu wa taarifa ya wafugaji
hao hakuna kilichofanyika mpaka sasa
Post a Comment