0

 Mwenyekiti wa chama cha ushirika cha Umoja (Umoja Amcos) ndugu Hasani Mpako akizungumza na wakulina na wanachama wa chama hicho septemba 24 katika viwanja vya Nanjinji kata ya Likongowele wilayani Liwale.
Wajumbe wa chama cha Umoja Amcos 


Mwenyekiti  wa chama cha ushirika cha Umoja (UMOJA AMCOS) ndugu Hasani Mpako awaonya wakulima na wanachama hicho wenye tabia ya  kuweka vipande vya matofari, kokoto na  mabibo kwenye magunia wakati wanapozipeleka kwenye maghala wakati wa kuuza.

Onyo hiyo aliitoa jana septemba 24, 2016  kwenye mkutano wa chama hicho kilichofanyika katika viwanja vya Nanjinji  kata ya Likongowele wilayani Liwale mkoani Lindi.

Ndugu, Mpako alisema moja ya changamoto wanazokutana nazo katika uongozi wa chama hicho baadhi ya wakulima na wanachama wanatabia ya  kuweka vipande vya matofari ,kokoto na  mabibo kwenye magunia wakati wanapozipeleka kwenye maghala wakati wa kuuza hali hii italeta sifa mbaya kwenye soko la mnada na kuonekana korosho za Liwale hazina ubora kwa uzembe wa watu wachache.

“Kuna watu wengine watumishi wa serikali tumewahi kuwakamata wameweka vipande vya matofari kwenye magunia ya korosho na wanakuja kuomba mchana na usiku tusiwapeke kwenye vyombo vya sheria watakosa kazi lakini sasa watu wenye tabia hii hatuwavumilia ” alisema Mpako.

Katika mkutano huo wanachama wa chama hicho kwa pamoja walikubaliana na kulidhia na  bei ya usafirishaji kutoka kwenye kituo wanachouzia na kusafirisha mpaka kwenye ghala kuu la mnada la chama hicho kila kilo moja watakata shilingi 20/= na kuwa na jumla ya ushuri zote kufikia shilingi 211 na wakulima hao watashirishwa wakati korosho hizo zitakapouzwa kwa mnada.

Mpako alisema jambo la ucheleweshaji  wa usafirishaji  kwenda kwenye soko la mnada hatarajii kujitokeza na mpaka sasa amepokea maombi  ya wasafirishaji  ya watu watatu na anatarajia kuwashawishi na watu wengine ili kuweza kuzifisha korosha kwenye soko kuu la mnada kwa wakati.

Mwenyekiti huyo akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa wanachama juu ya ucheleweshaji wa soko la mnada alisema swala la kuchewa mnada ni gumu na halina jibu la moja kwa moja kikubwa kuomba wanunuzi waje kwa wingi Pia katika mkutano huo Mpako aliwasisitaza wakulima kufungua akaunti banki.

Post a Comment

 
Top