0

 Celtic hawakuweza kumdhibiti Messi

Celtic walipokezwa kichapo kibaya zaidi katika mashindano ya Ulaya Jumanne usiku baada ya kuchapwa mabao 7-0 na Barcelona uwanjani Camp Nou.

Mshambuliaji Lionel Messi, raia wa Argentina, alifunga 'hat-trick' yake ya sita katika mechi hiyo ya kundi C.

Alianza kwa kufunga bao la mapema.

Mchezaji wa Celtic Moussa Dembele alishindwa kufunga penalti kabla ya Messi kufunga la pili.

Kipindi cha pili, Neymar alifunga kupitia frikiki, Andres Iniesta akafunga la nne, Messi akaongeza la tano naye Suarez akakamilisha ushindi kwa mabao ya sita na saba.
 Neymar baada ya kufunga bao la tatu Camp Nou

Katika misimu miwili ambayo wamekuwa pamoja Nou Camp, Messi, Neymar na Luis Suarez wamefunga mabao 253 na kusaidia ufungaji wa mabao 120.
 Andres Iniesta alifunga baada ya kuingia kama nguvu mpya

Post a Comment

 
Top