0

Zikiwa zimepita siku 67 tangu abebe majukumu ya kuinoa England, Sam Allardyce kwa ridhaa yake ameamua kujuzulu nafasi yake ya umeneja kufuatia shutuma nzito za kuonekana kwenye video akitoa ushauri wa jinsi wa kupindisha sheria za usajili za FA, imethibitishwa.
Baada ya uamuzi huo, bosi wa kikosi cha England cha chini ya miaka 21 Gareth Southgate atashikilia wadhifa huo kwa muda na kuiongoza timu hiyo kwenye michezo minne ijayo, michezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Malta, Slovenia na Scotland, na ule wa kirafiki dhidi ya Uhispania.
Mtandao wa The Daily Telegraph lilichapisha kipande cha video kilichodaiwa kumwonesha Allardyce akiwaambia watu wawili ambao wanahisiwa kuwa ni kutoka Mashariki ya Mbali kwamba angewapa mbinu ya kupindisha sheria za usajili wa wachezaji za FA kwa kutumia njia ya ‘third-party ownership’.
Ametuhumiwa kufikia makubaliano ya kulipwa kiasi cha euro 400,000 ili kuwasaidia katika mchakato huo wa uvunjaji sheria na kuahidi kuwawaklisha katika baadhi ya matukio ambayo yangehodhiwa na FA.
Allardyce ,61, pia ametuhumiwa kumkosoa mtangulizi wake kwenye kiti cha umeneja wa England Roy Hodgson na msaidizi wake Gary Neville kufuatia England kutolewa na Iceland kwenye Michuano ya Euro 2016, huku akishindilia msumari mwingine kwa kusema kitendo cha FA kutumia gharama kubwa kuufanyia marekebisho Uwanja wa Wembley ni “upuuzi”.
Allardyce anazidi kuhas England manager’s disease
“FA inathibitisha kwamba Sam Allardyce ameacha nafasi yake kama meneja wa England,” taarifa rasmi ya FA imeeleza.
“Kitendo alichokifanya Allardyce, kama ilivyoripotiwa leo, hakikuwa cha kiungwana hasa kwa meneja wa England. Amekubali kwamba amefanya kosa kubwa na tayari ameomba radhi. Hta hivyo kutokana na ukubwa wa shutuma, kwa pamoja FA na Allardyce wameamua kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba mara moja.
“Huu si umamuzi ambao umechukuliwa kijuu-juu isipokuwa baada ya kufikiria kwa kina ili kulinda maslahi mapana ya mchezo wa soka na kuendelea kuufanya mchezo kuendelea kuwa na heshima kubwa.
“Meneja wa timu ya England ya wakubwa lazima adumishe misingi imara ya nidhamu na kuonesha heshima katika mchezo wa soka kwa nyakati zote.
“Gareth Southgate atachukua nafasi hiyo na kusimamia michezo ijayo dhidi ya Malta, Slovenia, Scotland na Uhispania wakati huo FA ikianza mchakato wa kusaka kocha mpya.
“FA inapenda kumtakia Sam kila la heri kwa siku zijazo.”

Post a Comment

 
Top