Afisa
Uhusiano na matukio wa Airtel Tanzania, Dangio Kaniki akiongea na
waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mafanikio ya mafunzo ya
stadi za ufundi yanayotolewa na VETA kupitia mtandao wa simu ya mkononi
wa Airtel yajulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO katika ofisi za
makao makuu ya Airtel Tanzania zilizoko Moroco jijini Dar es Saalam hapo
jana.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa kijamii wa Airtel
FURSA ikishirikiana na Mamlaka ya elimu ya ufundi Tanzania (VETA)
imeendelea kuwawezesha vijana kupata kozi mbalimbali zinazotolewa katika
vituo vya VETA nchini kupitia application ijulikanayo kama “VSOMO”
yaani VETA SOMO.
Akiongea
na waandishi habari afisa Uhusiano wa Airtel Dangio Kaniki alisema,
“vijana wameufurahia sana mpango huu unaowawezesha kusoma masomo kutoka
VETA kwa urahisi zaidi na kuchochea kukua kwa elimu kwa vijana wengi na
kuwawezesha kupata ujuzi wa ufundi na biashara itakayoongeza ufanisi
wao”.
“Mafunzo
kwa njia ya mtandao ni rahisi na yatapatikana kwa wateja wa Airtel
wenye simu zenye mfumo wa android. Mteja atatakiwa kupakua application
ya VSOMO kwenye orodha ya menu yake ya simu sehemu ya google play store
na kujiandikisha bure. Mara baada ya kumaliza masomo yake kwa 40%
mwanafunzi atatakiwa kwenda kwenye kituo cha VETA kilichopo karibu nae
na kujiandikisha kwaajili ya mafunzo kwa vitendo ambayo yatachukua muda
wa wiki 2 kumaliza ikiwa ni sawa na masaa 60 na ndipo atakapokaa
kwaajili ya mtihani na kutakiwa kufaulu kwa 60% “alisisitiza Kaniki.
Aliendelea
kusema kuwa “vijana zaidi ya 19000 wamejisajili kusoma kozi mbalimbali
kutoka VETA kupitia simu zao za mkononi. Kwasasa masomo yanayopatikana
ni Ufundi pikipiki (bodaboda), Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi wa
simu za mkononi, Ufundi Alluminium, utaalamu wa maswala ya urembo na
ufundi wa kuchomelea vyuma.”
Akibainisha
hayo Kijana Saleh Shomari anayesoma kozi ya ufundi umeme kupitia
application ya VSOMO alisema “ VSOMO imekuwa msaada kwangu maana
nilikuwa natamani kusoma kozi VETA lakini sikuwa na mda wa kufika chuo
cha VETA kutokana na mihangaiko ya biashara zangu, lakini nawashukuru
Airtel na VETA kulionahili na sasa najisomea mafunzo haya ya umeme jioni
nikishafunga biashara yangu na kuweza kufikia malendo yangu ya kupata
cheti kutoka VETA.”
Dangio
alimalizia akisema” Mwanafunzi atatahiniwa na kisha kuandikishwa na
kutakiwa kulipia kiasi shilingi 120,000/= kwa kupitia Airtel Money kwa
kupiga *150*60# kama gharama ya mafunzo hayo. Tunatoa wito kwa vijana
kutumia fursa hii ya kipekee ili kupata mafunzo ya ufundi kwa urahisi na
gharama nafuu kwani gharama ya masomo iko chini zaidi.”
Post a Comment