ABIRIA wa mabasi ya kwenda mikoani na nchi jirani katika Kituo
cha Ubungo (UBT), wa- natozwa viingilio batili kiny- ume cha utaratibu.
Utaratibu unaojulikana abiria anapokuwa na tiketi hairuhisiwi kumtoza fedha za kiingilio ambayo ni Sh 300. Hata hivyo, hali ni tofauti kwani watu wote wamekuwa wakitozwa fedha za viingilio. Wakizungumza na MTANZANIA kwa nyakati tofauti, abiria hao walisema wameshangazwa na utaratibu huo,kwani siku zote wanaposafiri huingia katika kituo hicho kwa kutumia tiketi za mabasi wanayosafiria.
Mmoja wa abiria hao Angela Yoredi aliyekuwa akisafiri kuelekea Dodoma na basi la ABC alisema ilimpasa kulipia kiingilio cha Sh 200, licha kuonesha tiketi yake mlangoni.
“Nashangaa imebidi nilipie Sh 200 wakati siku zote nikiwa na tiketi ya basi ninapita bila kulipia, waliniambia huo ni utaratibu mpya unaotumika kwa sasa,” alisema Angela.
Naye Mohamedi Issa ambaye alikuwa anasafiri na basi la Hood kwenda Morogoro alisema kwa sasa utaratibu wa kuingia katika kituo hicho haueleweki, kwani awali watu waliokuwa wanalipa ni wale waliokuwa wakiingia kituoni kwa ajili ya kupokea au kusindikiza abiria.
“Utaratibu wa humu sasa haueleweki pale mlangoni kuna abiria wanalipa Sh 200 lakini mimi nililipa Sh 300 in- gawa nilikuwa tayari na tiketi yangu ya basi,” alisema.
Akitoa ufafanuzi wa suala hilo, Ofisa Uzalishaji, Uratibu na Ushuru kituoni hapo, Novat Francis, alisema kitendo hicho ni kinyume cha sheria na uta- ratibu ambao umepangwa katika kituo hicho.

Post a Comment