0


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) akiongoza kikao baina ya Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira ya Zanzibar. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Wataalam kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) na Mamlaka ya Udhibiti wa shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA).
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Hassan Mbarouk, akiongea jambo wakati wa kikao baina ya Wizara ya Nishati na Madini na baadhi ya Taasisi na Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati na Mazingira kilichojadili Utafutaji wa Mafuta na Gesi kwenye maeneo ya Bahari ya Hindi.
Wajumbe wa kikao wakifuatilia kikao baina ya Wizara ya Nishati na Madini na Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati na Mazingira ya Zanzibar. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati na Mazingira Zanzibar. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Nishati Zanzibar, Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati na Mazingira Zanzibar.
Mtaalam kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzani, akiwaonesha wajumbe wa kikao ramani inayoonesha maeneo ya shughuli za Utafiti wa Mafuta na Gesi nchini.

………………………

Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati na Mazingira ya Zanzibar, wamekutana katika kikao kilichojadili Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia kwenye maeneo ya Bahari ya Hindi.

Kikao hicho kimejadili kuhusu umuhimu wa kuimarisha mahusiano na ushirikiano zaidi katika sekta ya nishati ambayo ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi.

Pia, mbali na kujadili suala la utafiti wa Mafuta na Gesi asilia, kikao hicho kimejadili masuala ya nishati ya umeme kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar. Aidha, Taasisi nyingine zilizoshiriki katika kikao hicho ni Watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA)

Post a Comment

 
Top