Msajili
wa Vyama vya Siasa, Jaji Mstaafu Francis Mutungia akisisitiza juu ya
umuhimu wa mkutano wa vyama vya siasa utaofanyika Septemba 3 hadi 4 mwaka huu jijini Dar es Salaam mkutano uliofanyika katika Ofisi Msajili
wa Vyama vya Siasa leo jijini Dar es Salaam.
Makamu
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa,Vuai Ali Vuai akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kusogeza mkutano wa vyama
vya siasa leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mjumbe na Mwenyekiti wa
kamati ya fedha ya baraza la vyama vya siasa, Constatine Akitanda.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
BARAZA
la vyama vya Siasa nchini limesogeza mbele mkutano wa kujadili
sintofahamu iliyojitokeza kwa baadhi ya vyama vya siasa na kusababisha
kuwepo kwa hofu, na taharuki kwa wananchi.
Mkutano huo ulitangazwa kufanyika Agosti 29 hadi 30 na kusogezwa kufanyika Septemba 3 hadi 4 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Baraza
la Vyama vya Siasa, Vuai Ali Vuai amesema kusogeza mbele kwa mkutano huo
kumetokana na kutaka kutoa muda kwa wadau ili waweze kujiandaa.
Amesema
kuwa mkutano huo ni muhimu sana kwa wadau kukutana na kujadili mambo
yaliyojitokeza na kuweka sawa kwa mstakabali wa taifa.
jukwaa
la viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa kukutana mara kwa mara
kujadiliana masuala yanayohusu demokrasia ya vyama vingi na siasa hapa
nchini kwetu.
Amsema
kila chama cha siasa kinawakilishwa na viongozi wawili wa ngazi kitaifa
katika Baraza la Vyama vya Siasa, ambapo kiongozi mmoja anapaswa kutoka
Tanzania Bara na mwingine Zanzibar.
Mwenyekiti
na Makamu mwenyekiti wa Baraza huchaguliwa miongoni mwa wajumbe wa
Baraza. Baraza la Vyama vya linaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za
zilizotungwa na Baraza.
Baraza
la vyama vya siasa lina majukumu ya kuishauri msajili wa vyama vya
siasa kuhusu migogoro baina ya vyama vya siasa,kumshauri Msajili wa
vyama vya siasa kuhusu masuala yenye masilahi ya kitaifa yanayohusu
vyama vya siasa na hali ya siasa nchini.
Aidha
amesema kazi ya baraza hilo kuishauri Serikali kupitia Msajili wa Vyama
vya Siasa kuhusu kutungwa, marekebisho na utekelezaji wa sheria ya
vyama vya siasa na sheria nyingine zinazohusu vyama vya siasa,kushauri
kuhusu uratibu wa shughuli za vyama vya siasa.
Baraza
hilo linaweza kumtaarifu Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu masuala
yoyote yanayohusu utendaji wa chama chochote cha siasaKamati ya uongozi
ya Baraza la Vyama vya Siasa inaundwa na Mwenyekiti wa Baraza, Makamu
Mwenyekiti wa Baraza, wenyeviti wa kamati nne za Baraza na katibu wa
Baraza.
Post a Comment