Tetesi za muda mrefu
hatimae leo August 30 2016 klabu ya Arsenal ya England inayofundishwa na
kocha mfaransa Arsene Wenger imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa
kimataifa wa Hispania aliyekuwa anaichezea Deporivo La Coruna Lucas
Perez.
Arsenal inaripotiwa kukamilisha usajili
wa staa huyo na kumleta Emirates kwa dau la pound milioni 17.1 ambazo ni
zaidi ya bilioni 49 za Kitanzania, Perez amejiunga na Arsenal kwa
mkataba wa miaka minne.
Perez mwenye umri wa miaka 27 aliifungia
Deportivo La Coruna magoli 17 katika mechi 37 msimu uliopita, hata
hivyo kocha Wenger anaripotiwa kujiandaa kutangaza kumsajili beki wa
kimataifa wa Ujerumani anayeichezea Valencia Shkodran Mustafi dau
linalofikia pound milioni 35.
Post a Comment