Baadhi ya mabweni ya
shule kuungua katika mkoa wa Arusha na manyara imekuwa ikiendelea ambapo
katika mkoa wa Arusha jeshi la polisi kupitia kwa kamanda Charles
Mkumbo aliviambia vyombo vya habari kwamba kwa Arusha mpaka sasa hivi ni
mabweni ya shule sita ndio yaliyoungua.
Aidha
idadi ya shule ambazo zinakuwa zimekumbwa na matukio hayo iliongezeka
Jana August 29 2016 ambapo bweni la shule ya Aldasgate wilayani babati
mkoani manyara limeungua, tukio hilo limekuwa ni la pili kwa mkoa wa
manyara. Kamanda wa polisi Manyara Fransis Jacob amesema……….
>>>’Bweni
moja liliwaka moto na hivyo kuteketeza baadhi ya vitu vya wanafunzi
lakini kwenye vyumba hivyo viliweza kuokolewa lakini baadhi, kama
asilimia 80 ya vitu viliweza kuokolewa, bado tunafanya uchunguzi kujua
chanzo chake’
Tukio hilo la shule ya Aldasgate
linafanya matukio ya kuungua kwa shule kwa kanda ya kaskazini kufikia
nane ndani ya kipindi kifupi.
Post a Comment