0
 
 Mchezaji wa timu ya Kibutuka fc akigawa basi angalau aweze kupata bao katika kipindi cha kwanza



 Mwenyekiti wa chama cha msingi Umoja Amcos,Bwana Hasani Mpako aliyevaa kapelo ambaye aliyefadhili ligi ya Alizeti cup
 Mchezo wa uliokuwa na watazamaji wengi kutoka kila viunga vya mji wa Liwale

 Kocha wa timu ya Kibutuka fc,Maulidi Mnonya akitoa maekelezo kwa mchezaji wake angalau aweze kupata kupata ushindi lakini jitihada ziligonga ukuta 
 Timu ya Kibutuka fc ikipiga mpira wa adhabu ndogo baada ya kuchewa vibaya na beki wa timu ya Hawili fc
Mashabiki wa mpira waliokuwa wanafuatilia mchezo hatua kwa hatua 

Ligi ya Alizeti Cup leo August 30 2016 imeanza rasmi kutimua vumbi kama kawaida kwa mchezo mmoja  michuano hiyo timu ya Hawili fc  kucheza mchezo wake wa ufunguzi dhidi ya Kibutuka fc katika uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
Mchezo wa kwanza kwa Hawili fc katika hatua ya robo fainali wakati Kibutuka fc huu ni mchezo wa kwanza pia toka hatua ya makundi katika kanda zilipofuzu kuingia hatua ya robo fainali katika mchezo huo Hawili fc wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 5-3.
Magoli ya Hawili fc yalifungwa na Ramadhani dakika ya 9,Lawrence Fusi dakika ya 10,Imani Mbesigwa dakika ya 40 na Imani Mbesigwa dakika ya 81 na Magoli ya Kibutuka fc yalifungwa na Lemu Mneka dakika ya 36,Miraji Mtabiage dakika ya 86 na goli la 3 lifungwa Juma Hashimu dakika ya 88 ya lala salama baada ya kocha wa Kibutuka kufanya hisabu sana ndio aliweza kupata magoli.
 
Kocha wa timu ya Kibutuka fc,Maulidi Mnonya akizungumza na Liwale Blog alisema wameshindwa kupata upashindi kutokana na hali mbaya ya uwanja hivyo imewaharibu kisekolojia aliongeza kusema walikosa maandalizi ya mchezo yalikuwa mafupi.
 
Nae kocha wa Hawili fc,Mohamedi Farijala alisema anashukuru kwa kuibuka na ushindi wa magoli 5 kwa 3 licha ya ushindi huo aliwatupia lawama waamuzi wa mchezo huo na ameomba waamuzi waweze kuzingatia na kufuata sheria za mchezo ili kuweza kuchezesha mpira kwa mujibu wa sheria.

Agosti 31 kutakuwa na mchezo mmoja kati ya timu ya New Boys dhidi ya Super star mchezo unaotarajia kupigwa uwanja wa wilaya ya Liwale majira ya saa 10 jioni.

Post a Comment

 
Top