August 30 2016 klabu ya FC Barcelona ya Hispania imetangaza kukamilisha usajili mshambuliaji wa Valencia Paco Alcacer, FC Barcelona imetangaza kumsajili Paco kwa mkataba wa miaka mitano.
Paco ambaye ana umri wa miaka 23 anasajiliwa kwa dau la pound milioni 25.5 kutokea Valencia, lakini kama utakuwa unakumbuka vizuri Paco Alcacer anakuwa nyota wa sita kusajiliwa na FC Barcelona katika dirisha hili la usajili baada ya Jasper Cillessen, Andre Gomes, Samuel Umtiti, Lucas Digne na Denis Suarez.
Post a Comment