0

Arusha. Serikali imepewa Sh378 milioni kama mrabaha na madawati 500 kwa Mkoa wa Manyara baada ya Kampuni ya Tanzanite One kuuza madini ya Tanzanite.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo inayoendeshwa kwa ubia na Kampuni ya Sky Associate Limited na Shirika la Madini la Taifa  (Stamico), Faisal Shabhai amesema hivi karibuni waliuza madini yenye thamani ya Sh7.3 bilioni.

Shabhai amesema kampuni hiyo ambayo inamiliki Kitalu C katika machimbo ya Tanzanite Mirerani, ilipata faida katika mnada wa madini hayo uliofanyika mkoani hapa.

Akizungumzia madawati, amesema kampuni hiyo imetoa madawati 500 yenye thamani ya Sh35 milioni ili kumaliza tatizo la upungufu wa madawati katika Mkoa wa Manyara.

Post a Comment

 
Top