0

Agosti 2, 2016 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea Kiwanda cha Kuzalisha Sukari cha Mtibwa, kuangalia kiwanda chenyewe na kupata Maelezo kwa nn kiwanda hicho hakizalishi Sukari

Aidha alitembelea eneo ambalo linaendelea kupanuliwa kwa ajili ya mashamba ya miwa ikiwa ni pamoja na kutembelea ujenzi wa mitambo ya kusukuma maji kutoka Mtoni hadi kwenye mashamba ya miwa.

Hayo yote yalifanyika baada ya kupewa taarifa na uongozi wa kiwanda ambao  umeomba Serikali iwasaidie masuala kadhaa kama; kuwahakikishia Udhibiti wa Sukari inayoingizwa kutoka nje ya nchi na wanaoingiza watozwe kodi ili kuwa na ushindani sawa katika kuiuza kwa wananchi.

Wameiomba Serikali pia kuzibamyanya ya uingizaji wa sukari kwa njia za panya.
Kuvutiwa umeme wa KV zaidi ya 32, Serikali kudhamini viwanda Mara wanapotaka kukopa fedha Bank za nchi za nje, kujengewa Daraja la Dakawa, kuomba mashirika ya Kijamii kuwekeza katika viwanda nk.

Mwisho Mhe. Waziri Mkuu aliwahutubia wananchi wa Tuliani na muwata kufanya kazi kwa bidii, kusaidia azma ya Serikali  ya ukusanyaji wa kodi ktk maana ya kutoa na kudai risiti kwa kila kitu Mwananchi anachouza/kununua. Pia alisisitiza kutotoza ushuru kwa wafanyabiashara wadogo.

Wananchi nao kupitia Mbunge wao Mhe. Saddiq waliwakilisha kero zao zikiwemo: gharama kubwa ya madawa ktk Hospitali Teule ya Bwagala, migogoro baina ya wakulima na wafugaji, mahusiano hafifu na kiwanda cha Sukari cha Mtibwa n.k.

Kuhusu gharama ya madawa kuwa kubwa hospitali ya Bwagala ameahidi kumtuma Waziri Mwenye dhamana kuja kulitatua. Kuhusu migogoro ya wakulima na wafugaji amerudia mpango uliopo wa Serikali wa kutumia Ranchi zote kuzigawa ktk Blocks na kugawa kwa wafugaji kadri ya idadi ya mifugo. Kwa sasa ameshauri kuwa kila upande uheshimu Mali ya mwenzake na anayekiuka agizo hilo sheria ichukue mkondo wake.

Kuhusu mahusiano kati yao na kiwanda amekitaka kiwanda Kujitahidi kuweka mahusiano mema na wananchi kwa kushawishi Out growers kuendelea kulima miwa lakini kiwanda kinunue miwa yao bila kuwanyonya.

Lakini pia kulipa malipo wanayodai na wakylima, wafanyakazi na wastaafu. kuwaletea wananchi maendeleo yao ikiwa ni pamoja na kushirikiana katika masuala ya kijamii kama kujenga shule, hospitali, maji nk.

Kabla yakuongea na wananchi hao kulikuwa na zoezi la kupokea madawati 880 kutoka kwa wakala wa Misitu TFS ambapo Mhe.Kassim Majaliwa aliyakataa madawati 84 kati ya yale yaliyoletwa uwanjani hapo kwa kuwa hayakuwa na ubora uliohitajika na kuyataka yarudishwe kwenye karakana kutengenezwa kufikia ubora unaohitajika.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ameutaka Uongozi wa Serikali ngazi  ya Mkoa wa  Morogoro na Wilaya ya Mvomero kuhakikisha inaondoa vikwazo vyovyote vitakavyojitokeza kukwamisha Kiwanda cha nyama cha Nguru Hills kutofikia malengo yake.

Mhe. Majaliwa ametoa agizo hilo Leo alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Wilayani Mvomero Mkoani hapa.

Amesema kiwanda hicho pamoja na kuliongezea pato taifa lakini pia kitatoa ajira kwa vijana takribani 300 na kuondoa migogoro kati ya wakulima na wagugaji.

"Kiwanda hiki kitasaidia kuondoa migogoro baina ya wakulima na wafugaji kwa kushawishi wafugaji kuuza mifugo yao katika kiwanda hiki kwa bei yenye tija na hivyo kupunguza ukubwa wa migogoro katika Mkoa wa Morogoro" amesema.

Hata hivyo ameitaka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Kutoa elimu kwa wafugaji  kukubali na kutekeleza azma ya Serikali ya kutaka Ranchi zote za taifa kugawanywa ktk Blocks na kutolewa kwa wafugaji ili wafuge mifugo yao kwa tija na hivyo kuepusha migogoro inayojitokeza.

Kwa upande wa wananchi wanaozunguka kiwanda hicho cha nyama amewataka kutoa ushirikiano na kuwa walinzi wa kiwanda kwa kuwa kina manufaa kwao na kwa Taifa ikiwemo ajira, kuondoa migogoro iliyopo sasa kununua mazao yao kwa ajili ya kunenepesha mifugo inayotarajiwa kuchinjwa kiwandani hapo na kiwanda kusaidia masuala ya mengine ya kimaendeleo kama afya, elimu maji n.k.

Kiwanda cha Nguru Hills kinatarajia kukamilika Mwezi Disemba mwaka huu na kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa Kuchinja ng'ombe 300 na mbuzi 1500 kwa Siku.

Mhe. Waziri Mkuu amekamilisha ziara yake ya siku tatu Mkoani hapa kwa kutembelea kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha msamvu ambacho kinatarajiwa kukamilika wiki mbili zijazo.

Post a Comment

 
Top