Mapenzi
ni kitu kitamu sana hapa duniani na hata hupelekea mambo mengine
yasiyohusiana na mapenzi moja kwa moja kuwa kwenye mstari nyoofu iwapo
tu utakuwa unapendwa na kupenda pia.
Na mapenzi ni kitu kibaya sana kama utafanya kinyume na itarajiwavyo
kwenye mahusiano na huweza hata kusababisha mambo mengine yasiyohusiana
na mapenzi kwenda mrama/kombo.
Yafuatayo ni baadhi ya makosa ambayo unaweza kuyafanya ukidhani ni
madogo sana lakini kwa wengi hupelekea mahusiano kuvunjika mara moja na
kubaki unajuta na kulaumu kwa kile ulichofanya na ambacho ungeweza
kukizuia wewe mwenyewe;
PUNGUZA KUJALI Hakuna
kitu kinachovunja mapenzi kirahisi kama iwapo tu ulikuwa unajali sana
mwanzo wa mapenzi yenu lakini ghafla ukapunguza kumjali mwenza wako na
kuanza kufanya vitu tofauti na matarajio yake. Hakuna kitu kizuri kwenye mapenzi kama careness kwa mpenzi wako, hurefusha mapenzi sana na tofauti na hapo mapenzi huvunjika.
KUWA MLALAMISHI Hii
ni kitu nyingine kibaya sana kwenye mahusiano, hakuna mtu anayependwa
kusikia mwenza wake analalamika tu kila siku. Ukiwa ni mtu wa kupenda
kulalamika sana kwenye mahusiano basi kuna hatari sana ya kuja kukimbiwa
mbeleni na umpendaye siku akichoka hiyo tabia.
ACHA WIVU Kuna
msemo unasema ‘’hakuna mapenzi bila wivu’’. Hii inaweza kuwa kweli kwa
namna moja ama nyingine. Ulishazoea kuonyesha wivu kwa mpenzi wako
lakini ghafla siku hizi unachukulia poa kila kitu na hata huna wivu hata
afanye kitu ambacho ungeonyesha wivu, hapo lazima kutakuwa na ‘’doubt’’
na itapelekea kuchunguzwa na mwenza wako na mwishowe atagundua vitu
vitakavyopelekea uhusiano kufa.
KUWA BIZE Hiki
ni kitu hatari sana kwenye mapenzi na huwatokea wengi sana hasa wale
wafanyakazi na wafanyabiashara wakubwa, wapo bussy sana kiasi kwamba
wanakosa hata muda wa kukaa na wenzi wao na kufahamu mengi kuhusu
uhusiano wao.
SALITI Hiki
ni mojawapo ya vigezo hatari sana kwenye mahusiano ambavyo husababisha
wengi kuachana na kuanza maisha mapya ya kimapenzi bila wawapendao
kuwepo, mwenza wako akigundua kuwa umem-cheat huumia sana na ni wachache
sana huweza kuvumilia na kusamehe lakini wengi huchukua maamuzi ya
kuondoka.
KOSA MSIMAMO Hii
pia husababisha wenza wengi kukimbia iwapo tu uliyenaye kwenye
mahusiano ataonyesha kuanza kukosa msimamo kwenye mapenzi yenu. Hii hali
huogopesha wengi na kuamua kukimbia na kuanza maisha mapya kimapenzi na
mwingine tofauti na wewe.
KUTOKUWA NA MALENGO Hakuna
mtu wa dunia ya sasa anayependa awe na mtu asiye na future ya maisha
yake binafsi wala ya maisha yao kama wapenzi. Si msichana wala mvulana,
wote siku hizi kabla ya kuwa na wewe huangalia kwanza kama wataweza
kuishi na wewe na je una akili yoyote ya kufikiria maisha ya baadae au
umejisahau unawaza starehe tu bila kujua kesho itakuwaje.
Post a Comment