0


Maelfu ya waokoaji wameendelea na zoezi la kutafuta manusura wa tetemeko la ardhi usiku wote wa jana nchini Italia

Maelfu ya waokoaji wameendelea na zoezi la kutafuta manusura wa tetemeko la ardhi usiku wote wa jana kufuatia tetemeko hilo lililotokea kwenye eneo la milimani la kati la Italia.

Zaidi ya watu 247 wameripotiwa kufa na karibu watu 368 wamejeruhiwa huku watu wengi zaidi wakiaminika kuwa bado wapo chini ya vifusi vya majengo.

Waokoaji 4,300 wanatumia mitambo ya kunyanyua vitu vizito pamoja na mikono kutafuta watu waliofukiwa kwenye vifusi, huku ikitahadharishwa kuwa vifo zaidi vinaweza kuongezeka.

Waziri wa Afya wa nchi hiyo amesema wengi wa wahanga wa tetemeko hilo la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha alama 6.2 ni watoto.

Post a Comment

 
Top