Viongozi wa chama
cha upinzani cha Chadema Nchini Tanzania walioshikiliwa jana jioni na
kuhojiwa na jeshi la polisi na baadaye kuachwa kwa dhamana, wanatarajiwa
kurudi tena kikuo kikuu cha polisi leo kwa maojiano zaidi.
Viongozi
hao walikamatwa jana jioni wakiwa kwenye Hoteli ya Girrafe iliyopo
mjijini Dar es salaaam wakifanya mkutano wa ndani ya chama hicho.
Kupanga mikakati ya kutekeleza kile wanachokiita Operasheni Ukuta.
Inayotarajiwa
kufanyika septemba mosi ikilenga kupinga kile wanachokiita ni kubanwa
kwa demokrasia kwa serikali ya awamu ya tano.
Polisi
waliwashikilia viongozi hao kufuatia kukiuka amri iliyotolewa na jeshi
la polisi mwishoni mwa juma lililopita kupiga marufuku mikutano yote ya
ndani ya vyama vya siasa.
Kufuatia mauaji ya askari polisi wanne yaliyotokea nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Waliokamatwa
ni mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, katibu mkuu Dk. Vicent
Mashinji, naibu Katibu mkuu bara John Mnyika na makamu mwenyekiti
Zanzibar Said Issa.
Post a Comment