Kundi la wapiganaji
la Islamic state limetangaza kuwa mmoja wa kamanda wake mwandamizi
ambae ni msemaji wa kundi hilo, Abu Muhammad al-Adnani ameuwawa nchini
Syria.
Taarifa ya mtandao unaohusiana na kundi hilo Amaq, inasema
kuwa Abu Muhammad ameuwawa wakati alipokuwa kwenye operesheni za
kijeshi katika jimbo la Allepo. Mtandao huo haukutoa taarifa nyengine zaidi.
Wanajeshi wa marekani wamethibitisha kuwa walikuwa wamemlenga Abu Muhammad al-Adnani lakini wanasema bado walikuwa wakichunguza matokeo ya shambulizi la anga la siku ya Jumanne katika mji wa Al-Bab, kaskazini mashariki ya jimbo la Allepo.
Marekani inamuelezea Abu Muhammad al-Adnani kuwa ni mpangaji mkuu wa mashambulizi ya nje ya I-S na imesema kuwa kifo chake kinaweza kuwa nukta muhimu ya kushindwa kwa kundi hilo.
Post a Comment