Tanzania
inakabiliwa na kiwango cha juu cha ukatili wa kijinsia ikiwemo ndoa na
mimba za utotoni, pamoja na vipigo kwa wanawake kutoka kwa waume zao
licha ya juhudi mbali mbali za kupinga hatua hiyo na sheria kali
kutungwa bado matukio ya aina hii yanazidi kuongezeka.
Utafiti wa
hali ya afya ya uzazi,mtoto na malaria wa mwaka 2015/2016 unaonesha kuwa
idadi ya wasichana wanaopata watoto katika umri wa miaka 15-19
imeongezeka mpaka kufikia asilimia 27 mwaka 2015 kutoka asilimia 23
mwaka 2010.
Kwa muujibu wa utafiti uliofanywa na UNICEF wa mwaka
2015,Tanzania ina asilimia 3.5 ya watoto wa umri wa miaka 7-17 walio
nje ya shule.
Hii inajumuisha watoto takriban milioni 2 walitakiwa
kuwa shule za msingi na watoto takriban milioni 1.5 waliotakiwa kuwa
shule za sekondari.
Aidha utafiti huo umetanabahisha kuwa katika
kila watoto watano wa umri wa kuwa shule ya msingi,kuna mtoto ambaye
hayuko shuleni na katika kila watoto watano wa umri wa kuwa shule ya
sekondari kuna watoto zaidi ya wawili ambao hawako shuleni kutokana na
sababu mbali mbali.
Katika harakati za kutokomeza ndoa za utotoni,ukatili
wa kijinsia kwa mtoto wa kike na wanawake licha ya kuwapa mafunzo
maafisa maendeleo ya jamii ,maafisa ustawi wa jamii na hata polisi na
kuwajengea uwezo wasichana ,vilabu 350 vya wasicha vimeundwa nchini
Tanzania ambao wanatambua haki zao za msingi.
Post a Comment