Chama kikuu cha upinzani nchini Zambia kimepeleka
kesi mahakamani kupinga ushindi wa Rais Edgar Lungu uliofanyika mapema
mwezi huu.
Mgombea wake wa urais Hakainde Hichelema, aliiambia BBC
kuwa uchaguzi huo uliibwa kutoka kwake na haukuonyesha matakwa ya
watu wa nchi humo.
Chama chake cha National Development (UNDP)
kimemuandikia spika wa bunge, kikimtaka achukue wadhifa wa urais hadi
uamuzi wa mahakama utolewe.
Tume ya uchaguzi nchini Zambia
ilikuwa imemtangaza Lungu kuwa mshindi kwa asilimia 50.35 huku Hichilema
akipata asilimia 47.67 na kusisitiza kuwa uchaguzi ulikuwa wa haki.
Bwana Lungu alimshinda Hichilema uchaguzi uliotangulia mwaka uliopita kwa chini ya kura 28,000.
Post a Comment