0

RPC - CUP 2016
Timu ya Kata ya Rasibura wakikabidhiwa Kikombe na Kamanda wa Mkoa wa Lindi kutoka Takukuru Ndg. Chami baada ya Kuibuka washindi kwa kuifunga Timu ya Kata ya Makonde.
RPC - CUP 2016 D7 disantos
Hashimu Hamisi au D7 (anaefananishwa na Cristiano Ronaldo) akiwa na tuzo yake baada ya kuibuka mshindi wa Mchezaji Bora wa Mashindano ya RPC - CUP 2016 akiichezea Timu ya Kata ya Mnazi Mmoja. 
RPC - CUP 2016
Kikundi cha Ushangiliaji kutoka Rahaleo kikikabidhiwa Zawadi yao mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika Ligi ya RPC - CUP 2016 ambayo imemalizika jana ndani ya uwanja wa Ilulu.

Na. Mwandishi wetu, Lindi
Ligi ya RPC-CUP 2016 jana agosti 25 imefikia kikomo baada ya kupigwa mchezo mmoja wa fainali kati ya timu kutoka kata ya Makonde dhidi ya  Rasibura zote zikitokea Manispaa ya Lindi.

Mchezo huo ulioshuhudiwa na Mashabiki lukuki kutoka katika pande mbalimbali za Manispaa hiyo ulivuta hisia ya kipekee kwani timu hizo zilikuwa katika Kundi moja kabla ya fainali hiyo ambapo mchezo wa awali timu ya Makonde iliibuka kidedea lakini leo mambo yamekuwa ndivyo sivyo.

Fainali hiyo ilianza kurindima mnamo majira ya saa Kumi kamili za Jioni na hadi Kipyenga cha mwisho cha Mwamuzi wa mchezo huo kinapulizwa kuashiria mchezo umemalizika hakuna Timu iliyoona lango la mwenzie na kuamriwa kupigwa kwa mikwaju ya penati.

Makonde hawakuweza kuzitumia vizuri kwani waliweza kupata mkwaju mmoja tu kati ya Nne ya zile zilizo pigwa na Timu ya Rasibura kuweza kuitumia vizuri mikwaju hiyo kwani waliweza kufunga penati zote Nne na kuibuka washindi wa Fainali hizo.

Kamanda wa Mkoa wa Lindi kutoka Takukuru Ndg. Chami ambaye alikuwa ndiye mgeni rasmi wa Mchezo huo aliweza kukabidhi zawadi mbalimbali kutoka kwa washindi mbalimbali wa fainali hizo.

 Zawadi ya Mshindi wa Tatu ilikwenda kwa Timu ya Kata ya Mingoyo na kuweza kupata zawadi ya Medali za Shaba na Pesa kiasi cha Tsh 400,000.00 huku Mshindi wa pili ikienda kwa Timu ya Kata ya Makonde na kuweza kupata Medali ya Fedha na Pesa Tsh 600,000.00 pamoja na Kikombe

 Mshindi wa kwanza aliweza kuzawadiwa Kikombe Medali ya Dhahabu pamoja na Pesa tasilimu Tsh Milioni Moja (1,000,000.00).


RPC - CUP 2016
Kikosi cha Kwanza cha Timu ya Kata ya Makonde Kilichocheza mechi ya Fainali dhidi ya Timu ya Kata ya Rasibura jana ndani ya Uwanja wa Ilulu. 
RPC - CUP 2016
Kikosi cha Kwanza cha Timu ya Kata ya Rasibura  Kilichocheza mechi ya Fainali dhidi ya Timu ya Kata ya Makonde jana ndani ya Uwanja wa Ilulu. 
RPC - CUP 2016
Waamuzi wa Mchezo wa Fainali ya RPC - CUP 2016

Post a Comment

 
Top