0

Dirisha la usajili kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya SokaTanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili msimu wa 2016/2017 lilifungwa saa 6.00 usiku wa Jumamosi Agosti 6, 2016.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linasubiri utetezi wa Yanga kuhusu kushindwa kwao kutuma usajili wao wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara.

Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa amesema kwamba, klabu zote ambazo hakuzituma usajili wake, zinatakiwa kuandaa utetezi utakaokwenda TFF ambao utatumwa FIFA yenye mamlaka ya kufungua dirisha, na utetezi huo ukikataliwa timu husika inabidi ishuke daraja ambalo halimo kwenye usajili wa mfumo wa TMS.

TFF kwa sasa inasuburi barua ya utetezi wa klabu ambazo hazikukamilisha zoezi la usajili ili iutume FIFA, ambapo, sambamba na hilo TFF inatathimini mwenendo mzima kisha itatoa taarifa kwa FIFA ili kuangalia namna gani ya kushughulikia maeneo yaliyokuwa na upungufu kwa sasa na baadaye.

Post a Comment

 
Top