0

             Mchezaji wa timu ya polisi fc akikimbilia mpira kwa ajili ya kupiga basi
Ligi ya Alizeti cup indelea na michezo leo agosti 13 kulikuwa na mchezo mmoja kati ya ABAJALO dhidi ya POLISI FC mchezo uliopigwa uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
Katika kipindi cha kwanza timu ya polisi fc iliweza kupata goli la kuongoza lilofungwa na Mohamedi Saidi katika dakika ya 30 na goli hili lilidumu mpaka mapumziko dakika 45.
Katika kipindi cha pili timu ya polisi fc ilizidi kushambulia lango la timu ya Abajalo fc na kuweza kuongeza goli katika dakika ya 84 lilifungwa na Musa Musa.
Matokeo mpaka dakika 90 zinakamika ABAJALO FC 0-2 POLISI FC na kuifanya timu ya Abajalo fc kuweza kuagana na mashindano haya huku timu ya polisi fc ikisonga mbele ya mashindano haya.
 
Kocha wa Polisi fc Malijani Abdala alisema mchezo ulikuwa mzuri na katika mchezo wa leo timu ya Abajalo fc haikuwapa shida na kuweza kufanyikiwa kupata ushindi wa magoli 2 na kocho wa timu ya Abajalo fc Waziri Kasimu aliweza kuiambia Liwale Blog kuwa timu yake ni mara ya kwanza kushiriki ligi hivyo hawakuweza kujiamini wakati wakicheza lakini anajipanga upya ili kuweza kuondoa kasoro zilizojitokeza kuweza kuzisawazisha ili kuweza kufanya vizuri kwa mashindano yajayo.

Mchezo wa kesho agosti 14 unatarajiwa kuwa mkali na wakusisimua na kutarajia kuwa na mashabiki wengi kutakuwa na mchezo kati ya mabingwa wa Ligi ya Liwale super cup  SIDO FC ikiikaribisha timu ya  LIKONGOWELE CITY,timu ya Likongowele city imeweza kushiriki sana ligi mbalimbali hapa wilayani lakini haiwezi kuifunga timu ya Sido fc lakini mpira dakika 90 wenda ikawa maajabu.

Post a Comment

 
Top