Mkufunzi wa klabu
ya Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa ukosoaji uliotolewa na
kocha wa Arsenal Arsene Wenger na mwenzake wa Liverpool Jurgen Klopp
''hauna maadili''.
Wenger na Klopp wamelalamikia uhamisho wa pauni milioni 100 wa Paul Pogba.
''Kuna vitu ambavyo nikifanya havina maadili,lakini wengine wakifanya ni jambo la kawaida'',alisema Mourinho.
Mkufunzi
huyo wa United ameongezea kuwa atamsajili mchezaji mzuri wa kiungo cha
kati katika siku chache zijazo na Pogba ni muhimu.
''Kwa sasa tuna
wachezaji 22,alisema.Tutakuwa na 23.Ni mchezaji wa Juve hadi pale
atakapokuwa rasmi nje''.Soko la uhamisho linafungwa tarehe 31 mwezi
Agosti.
''Tunajaribu kila tuwezalo kufunga soko letu la ununuzi kwa haraka iwezekanavyo''.
Post a Comment