0

Sehemu ya manispaa ya Iringa


Manispaa ya Iringa imesitisha mkataba na mkandarasi wa barabara aliyepewa zabuni ya kujenga barabara katika kata tano ndani ya Manispaa hiyo baada ya kushindwa kutekeleza kazi hiyo kwa wakati.
Akizungumza katika kikao cha madiwani wa halmashauri hiyo mhandisi wa ujenzi wa manispaa, Mashaka Lihamba amesema mradi wa thamani ya zaidi ya shilingi milioni 60 ulikuwa unatekelezwa na kampuni ya Clients LTD ambae baadaye alitoroka eneo la kazi.

Lihamba ametoa ufafanuzi mara baada ya kupata malalamiko kutoka kwa madiwani wa kata hizo tano zilizokuwa zinahusika kwenye mradi huo ambao walishangazwa na mradi kusimama bila maelezo.

Kwa mujibu wa maelezo ya mhandisi huyo kuwa tayari wameshapata mkandarasi mwingine ambaye atamalizia mradi huo katika kata za Mlandege, Ilala, Makorongoni, Gangilonga na Mivinjeni.

Post a Comment

 
Top