Mchezaji wa soka ya
Marekani NFL amekataa kusimama ili kutoa heshima wakati ambapo wimbo wa
taifa unapoimbwa akipinga kile anachotaja ni ubaguzi wa rangi.
Colin Kaepernick ,anayeichezea timu ya San Fransisco 49ers alisalia akiwa ameketi wakati wimbo wa taifa ulipoimbwa.
''Sitasimama kujivunia bendera ya taifa linalokandamiza watu weusi na watu wengine wa rangi'',alielezea.
Mashabiki wengine walimzoma ,mchezaji huyo wakati alipoingia uwanjani.
Lakini
timu yake imesema kuwa inaheshimu haki yake ya kugoma wakati timu ya
49ers ilipokuwa ikikabiliana na Green Bay Packers katika mechi ya
kirafiki.
''Tunatambua uhuru wa mtu binafsi kujichagulia na
kushiriki katika sherehe za wimbo wa taifa'',timu hiyo ilisema. akipinga
kile anachotaja ni ubaguzi wa rangi.
Post a Comment