Mahakama moja
nchini Kenya imetoa uamuzi kwamba polisi wa utawala waliteka nyara
wakili Willie Kimani, mteja wake na dereva wa texi. Wote watatu
waliteswa na kuuawa, tukio ambalo lilisababisha maandamano nchini Kenya
dhidi ya mauaji yanayotekelezwa na polisi.
Mahakama ya juu
nchini kenya imegundua kwamba wakili Willie Kimani, mteja wake Josphat
Mwenda and dereva wa texi Joseph Muiruri walitekwa nyara mwezi Juni
Tarehe 23, wakazuiliwa katika kituo cha polisi ambacho hakijachapishwa
kwenye gazeti rasmi la serikali na ambacho kilitumika kuwatesa na kuuawa
kikatili.Mahakama hiyo pia imeamuru kwamba wakili Willie Kimani, hasa kwa sababu za vile aliuawa na mwili wake kutupwa mtoni, atambuliwe kama mtetezi wa sheria kama njia mwafaka ya kumkumbuka.
Jaji pia alifahamu kwamba uchunguzi wa mauaji haya uliingiliwa kati na washukiwa ambao walikuwa wamejitolea kusambaratisha haki kutendeka.
Chama cha wanasheria nchini Kenya kilikuwa kimewasilisha malalamiko mahakamani kikitaka polisi waseme kule wakili, mteja wake na dereva wa texi waliko wakati walipopotea.
Maafisa wanne wa polisi wa utawala tayari wameshtakiwa juu ya mauji haya.
Post a Comment