0


Guochuani Lai..
Klabu ya West Brom imenunuliwa na kampuni ya uwekezaji ya China iitwayo Yunyi Guokai (Shanghai) Sports Development Limited.

Kampuni hiyo ya uwekezaji inaongozwa na mwekezaji Guochuani Lai,42, mwenye hisa kubwa katika Yunyi Guokoi (Shanghai) Sports Development Limited.

Kufuatia timu hiyo kuuzwa Mwenyekiti wake Jeremy Peace ametangaza kuachia kiti hicho alichokikalia kwa miaka 14 na nafasi yake itachukuliwa na mwenyekiti wa zamani wa Blackburn John Williams.

Mwekezaji huyo mchina Guochuan Lai ambaye ni mmiliki mkubwa wa hisa wa kampuni hiyo ya uwekezaji,sasa ndiye atakuwa mmiliki mpya wa Klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza.

Post a Comment

 
Top