Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul makonda leo ameonyesha picha za
jengo kubwa la hospitali ya kinamama ambalo ujenzi wake tayari umeanza
kwa msaada kutoka Serikali ya Korea Kusini na linatarajiwa kuzinduliwa
na Rais Magufuli mwezi wa nne mwakani. Jengo hilo litakalogharimu jumla
ya shilingi bilioni 8 na milioni 800 litakuwa na uwezo kulaza wakinamama
(wagonjwa) 160 kwa wakati mmoja na litakuwa na chuo kwaajili ya
wanafunzi na tayari Madaktari kutoka Korea wamesha anzaa kutoa mafunzo
ya magonjwa ya kinamama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment