Bibi Sarah Cooke, Balozi mpya (Mteule) wa Uingereza nchini Tanzania amewasili 25 Agosti, 2016 Dar es Salaam.
Bi.
Cooke amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Bi.Dianna Melrose (ambaye
amestaafu) na ni mwanamke wa tatu kushika nyadhifa ya ubalozi
kuiwakilisha Uingereza nchini Tanzania.
Bi
Cooke alijiunga na Utumishi Uingereza mnamo mwaka 2002. Alifanya kazi
kadha wa kadha katika idara za Serikali ya Uingereza ikiwemo Shirika la
Kimataifa la Maendeleo la Uingereza (DFID), Wizara ya Mambo ya Nje na
Kitengo cha Mikakati cha Waziri Mkuu katika Ofisi ya Baraza la Mawaziri.
Pia alipata kuhudumu kama Makamu Mkuu wa Tume ya Sekretariati ya
Africa.
Hivi
karibuni, alikuwa ndiye Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo
(DFID) nchini Bangladesh. Kabla ya kujiunga Utumishi katika Serikali ya
Uingereza, alipata kufanya kazi kama Mchumi jijini London, Guyana na
visiwa vya Solomoni.
Juu
ya uteuzi wake, Bi.Cooke alisema; “Nimefurahi na ni heshima kubwa
kwangu kupewa jukumu hili jipya kama Balozi wa Uingereza nchini
Tanzania. Uingereza na Tanzania inafurahia mahusiano na ushirikiano wa
muda mrefu na kufanya kazi kwa karibu katika maeneo mengi ambayo
tunashabihiana katika vipaumbele ikiwemo biashara, uwekezaji, maendeleo
na usalama. Nina dhamiria kuimarisha ushirikiano huu bora zaidi na nina
taraji kuijua vyema Tanzania na watu wake”
Post a Comment