0


Picha zinazo muonyesha Bi. Sikuzani akiwa mwanae ambae ni mlemavu wa viungo wakiwa katika ofisi za afisa maendeleo ya jamii Wilaya Liwale, alipofika kwa ajili ya kuomba msaada.

 Picha zinazo muonyesha Bi. Sikuzani akiwa mwanae ambae ni mlemavu wa viungo
Fomu ya kuomba msaada wa kumchangia Bi. Sikuzani Ngwinde iliyotoka kwa Afisa Maendele ya Jamii Wilaya Liwale.


 Bi. Sikuzani Ngwinde mkazi wa Kijiji cha Mirui Wilayani Liwale anaomba msaada wa hali na mali kwa Watanzania wote mliojaaliwa kipato ili aweze kumhudumia mtoto wake mwenye ulemavu. Kwa mujibu wa Bi Sikuzani anasema kuwa mtoto wake ana umri wa mwaka mmoja na miezi tisa na alizaliwa na ulemavu kitendo kilichopelekea baba wa mtoto kumkimbia na hivyo kumfanya yeye ahangaike na mtoto wake bila msaada.

“Nimejitahidi sana kumhangaikia mwanangu peke yangu kwa kipindi kirefu hasa baada ya baba yake kunikimbia, nimetumia nguvu zangu nyingi ata ikafikia kuuza thamani zangu zote ili niweze kumhudumia mwanangu”Alisema Bi. Sikuzani huku akitokwa na machozi alipokuwa kwenye ofisi za afisa maendeleo ya Jamii Wilaya Liwale..

Kwa yeyote ambae ataguswa na kuhitaji kumsaidia Bi Sikuzani ili aweze kumtunza mtoto wake basi awasiliane na LIWALE BLOG kwa namba za simu 0656630250 na 0689286666
Kutoa ni moyo

Post a Comment

 
Top