Meneja Uhusiano na Ustawi wa Jamii wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya
Fahamu Muhimbili (MOI), Jumaa Almasi amesema kwa siku wanapokea wagonjwa
40 wengi wao wakiwa majeruhi wa ajali za bodaboda.Kauli hiyo imekuja
siku moja baada ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuitaka taasisi hiyo
kurejesha kambi za upasuaji ili kupunguza idadi ya wanaosubiri
upasuaji.“Awali walikuwa 20 kwa siku, lakini kwa sasa ni 40 na asilimia
80 ya wagonjwa hao wanahitaji upasiaji wa dharura na kiutaratibu, mwenye
dharura anahudumiwa mapema ili kuokoa maisha,” amesema huku akisisitiza
kuwa taarifa zilizoripotiwa kuhusu msongamano huo na kubana matumizi
siyo za kweli.
Lakini wakati Almasi akisema hayo, juzi, Waziri Ummy alifanya ziara ya kushtukiza MOI na kuagiza kambi za upasuaji zilizokuwa zikifanyika mwishoni mwa wiki zirudi mara moja ili kupunguza idadi ya wagonjwa wanaosubiri upasuaji.

Post a Comment