Leo July 23 2016 Rais John Pombe Magufuli amekabidhiwa rasmi nafasi ya uenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM
baada ya kupigiwa kura za ndio 2398 kutoka kwa wanachama wa chama
hicho ambapo hakuna kura hata moja ya hapana wala iliyoharibika
Baadhi ya
viongozi wakiwemo wa vyama vya upinzania walishiri akiwemo mwenyekiti wa
TLP Augustino Mrema, lakini wapo pia waliotamani kufikisha hisia zao
kuhusu tukio hilo na mmojawapo ni mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe
kupitia account yake ya facebook aliandika maneno haya…
>>>’Napenda
kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuwa Kiongozi wa
Chama chake cha CCM akiwa Mwenyekiti wa Tano chama hicho. CCM imeendelea
kudumisha utamaduni wa kukabidhiana Uongozi kila baada ya muda‘
‘Jambo ambalo ni la kujifunza hasa kwa vyama vya Siasa nchini na barani Afrika. Nataraji
kwamba Rais na Mwenyekiti mpya wa CCM ataona umuhimu wa Vyama vya Siasa
kuendelea kufanya Siasa bila vikwazo na kwa mujibu wa Sheria za Nchi
yetu.’ –Zitto Kabwe
‘Demokrasia inaimarisha Amani kwa kupaza sauti za HAKI. Karibu kwenye changamoto za kuongoza Vyama vya Siasa ndugu Rais.‘ –Zitto Kabwe
Post a Comment