Julai 23,2016 Taasisi ya Brigite
Foundation imezindua mradi wa taa za solar katika kituo cha walemavu wa
ngozi cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuimarisha
usalama katika kituo hicho ambacho sasa kina jumla ya watoto albino
220,wasiosikia 61 na wasioona 33.
Uzinduzi huo umefanywa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
ambapo mbali na uzinduzi huo wa mradi wa umeme mbadala,watoto katika
kituo hicho walishiriki michezo mbalimbali pamoja na kula chakula cha
pamoja na viongozi wa taasisi ya Brigitte Alfred Foundation na CSI
Electrical Limited (picha zipo hapo chini).
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo,Rais na Mwanzilishi wa
Brigitte Alfred Foundation bi Brigitte Alfred alisema mradi huo mkubwa
wa kisasa wa taa za sola utasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha usalama
wa watoto hao katika kituo hicho.
Brigitte ambaye ni Miss Tanzania mwaka 2012 alisema baada ya kuguswa na
hali iliyopo katika kituo hicho mwaka jana aliomba Kampuni ya
Wakandarasi wa Umeme wa ndani -CSI Kusaidia kufunga umeme katika kituo
hicho wakakubali na hatimaye leo mradi huo umezinduliwa.
“Tunaushukuru uongozi wa CSI Electrical Limited kwa namna walivyopokea
maombi yetu na hatimaye kuchukua hatua za haraka kwa kutoa msaada huu
pia viongozi wa serikali na chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi kwa
ushirikiano wenu uliosaidia kukamilika kwa mradi huu”,alieleza Alfred.
“Mradi huu umetimiza na kuunga mkono malengo ya Millenia namba 7
inayolenga upatikanaji wa nishati salama “Affordable and clean
energy”,tunatarajia mradi huu utahamasisha na kuchochea ari ya wanafunzi
katika elimu ya mazingira na matumizi ya nishati mbadala na
watawawezesha kusoma na kushiriki kwa vitendo katika kufikia malengo ya
kitaifa na ya kidunia kama kizazi na viongozi wa kesho”,aliongeza.
Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuiomba jamii kuunga mkono juhudi za
serikali na kusimamia kauli mbiu ya pamoja ya kuhimiza amani,upendo na
kutokomeza kabisa matukio maovu kwa watu wenye ulemavu wa ngozi na
kuifanya Tanzania endelee kuwa mahala pazuri na salama pa kuishi.
Kwa upande wake mwakilishi wa Kampuni ya wakandarasi wa umeme -CSI
Electrical Limited Joan Kahwa alisema wamefunga Panel 13 na mradi huo
umegharimu kiasi cha shilingi milioni 75.88.
“CSI ilipokea ombi la taasisi ya Brigitte Alfred Foundation kwa moyo
wote ili kuungana nao katika kuboresha maisha ya watoto wetu hapa
Buhangija,Mkurugenzi Mtendaji wa CSI Elecrical Limited alitembelea kituo
hiki mwaka 2015 ili kutafiti jinsi ya kukisaidia,katika ziara hiyo
tuligundua changamoto nyingi zinazowakabili watoto pamoja na walimu na
walezi waishio hapa kituoni”,alieleza Kahwa.
“Kwa awamu ya kwanza tuliona ni vyema kuboresha ulinzi wa eneo hili,kwa
kudhamini ununuzi,uingizaji,usafirishaji na ufungwaji wa taa za sola
shuleni hapa ili kuwe na mwanga wa kutosha nyakati za usiku”,alifafanua.
“Katika awamu ya pili tutalenga kuboresa mfumo wa maji ili upatikanaji
wa maji uwe rahisi zaidi kwa kufunga pump ya sola yenye uwezo wa kutosha
kwa kituo hiki,jitihada hii itasaidia kuboresha hali ya usafi katika
shule hii kwa kurahisisha shughuli za usafi,kufua,kuosha vyombo,kuandaa
chakula na usafi wa watoto kwa ujumla”,aliongeza Kahwa.
Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliyezindua mradi huo
aliipongeza taasisi ya Brigitte Alfred Foundation kwa kushirikiana na
kampuni ya wakandarasi wa umeme CSI Electrical Limited kufanikisha
kumaliza changamoto ya umeme katika kituo hicho.
Mkuu huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo kuwatahadharisha baadhi ya watu
wanaowinda watu wenye albinism kwamba serikali haitasita kuwachukulia
hatua huku akiwataka wazazi na walezi wa watoto hao kutowatekeleza
kituoni watoto hao.
Brigitte Alfred amefanikisha zoezi la kufunga umeme wa solar katika
kituo cha Buhangija mwaka mmoja tu baada ya kukamilisha ujenzi wa bweni
la kisasa la wanafunzi katika kituo hicho cha Buhangija mwaka 2015
linalowezesha kuishi watoto 70 ambalo lilizinduliwa na kukabidhiwa mwaka
2015.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,bwana Kadama Malunde alikuwepo
eneo la tukio ametuletea picha 60 za matukio yaliyojiri..Tazama hapa
chini
Mafundi umeme kutoka kampuni ya wakandarasi wa umeme CSI Electrical
Limited wanaojihusisha na kufunga umeme majumbani wakiendelea na zoezi
la kufunga mitambo ya umeme wa solar katika kituo cha watoto wenye
ulemavu wa ngozi (albino),wasiosikia na wasioona cha Buhangija katika
manispaa ya Shinyanga.
Mafundi umeme wakiendelea kufunga moja ya mitambo ya umeme unaotumia
nguvu ya jua katika kituo cha Buhangija...Kila mtambo una Panel 2 na
jumla ya Panel zilizofungwa katika kituo hicho ni panel 13,thamani ya
mradi wote ikiwa ni shilingi milioni 75.88
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa Umeme wa Solar katika kituo cha
Buhangija,Josephine Matiro akiwasili katika kituo hicho na kupokelewa na
watoto wanaoishi katika kituo hicho
Mwakilishi wa Kampuni ya wakandarasi wa umeme -CSI Electrical Limited
Joan Kahwa(katikakti) akimuonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro (kulia) akimuonesha moja ya mitambo ya umeme wa jua katika kituo
cha Buhangija.Kushoto ni Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred
aliyefanikisha kuwepo kwa mradi huo
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro na viongozi mbalimbali wakiangalia mtambo wa umeme wa solar
Mwakilishi wa Kampuni ya wakandarasi wa umeme -CSI Electrical Limited
Joan Kahwa akimuongoza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine kuangalia
mitambo ya umeme wa jua katika kituo cha Buhangija
Nyuma ya bweni lililojengwa na Miss Tanzania 2012 ,Brigitte Alfred
-Kushoto ni mratibu wa Brigitte Alfred Foundation Stanley Mosha
akimueleza mkuu wa wilaya kuhusu faida za mradi huo ambao utasaidia kwa
kiasi kikubwa kuimarisha ulinzi na usalama katika kituo hicho
Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia
mtambo wa umeme wa jua uliopo karibu na bweni lililojengwa na Miss
Tanzania 2012 Brigitte Alfred
Mkuu wa wilaya akiendelea kuangalia mazingira ya kituo cha Buhangija
Bweni lililojengwa na Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred
Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
akikata utepe ishara ya kuzindua mradi wa umeme wa Solar katika kituo
cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikata utepe.Uzinduzi huo
umehudhuriwa na viongozi wa taasisi ya Brigitte Foundation,viongozi wa
Chama watu wenye Ulemavu wa ngozi Tanzania (TAS),viongozi wa Kampuni ya
wakandarasi wa umeme -CSI Electrical Limited,wakuu wa idara ya elimu
makundi maalumu,mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga,walimu na watoto
wanaolelewa katika kituo hicho.
Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Buhangija Seleman Kipanya ambaye pia ni
msimamizi wa kituo cha watoto wenye ulemavu cha Buhangija akizungumza
ambapo alisema kituo hicho sasa kina jumla ya watoto 314
Rais na Mwanzilishi wa Brigitte Alfred Foundation bi Brigitte Alfred
akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo alisema mradi huo utakuwa
msaada mkubwa kwa maisha ya watoto hao kituoni hapo kwa ajili ya mwanga
Rais na Mwanzilishi wa Brigitte Alfred Foundation bi Brigitte Alfred
akitoa hotuba yake ambapo alisema Brigitte ameongeza kuwa mradi huo
utasaidia kituo hicho kuwa na umeme wa uhakika kwa gharama nafuu na
kuchochea ari ya wanafunzi katika elimu ya mazingira na matumizi ya
nishati mbadala.
Rais na Mwanzilishi wa Brigitte Alfred Foundation Brigitte Alfred
alisema taasisi yake inatambua uwepo wa vituo vingi vilivyo na mahitaji
tofauti mfano kituo cha Kabanga Kasulu mkoani Kigoma hivyo aliwahimiza
wadau mbalimbali kuungana pamoja katika kuwasaidia watoto.
“Naomba tuhakikishe kuwa watoto hawa wanarudi kujumuika,kuungana na
kushiriki na jamii katika ujenzi wa taifa kwa pamoja,kila mmoja wetu
ahakikishe anafanikisha kuwezesha watoto hawa wanajumuishwa katika jamii
na siyo vinginevyo,tunaomba vyombo vya habari kusaidia jitihada
hizi”,aliongeza Brigitte Alfred.
Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred akitoa hotuba yake
Miss Brigitte akiendelea kutoa hotuba yake
Miss Brigitte akifurahia jambo
Mwakilishi wa Kampuni ya wakandarasi wa umeme -CSI Electrical Limited
Joan Kahwa akielezea kuhusu mradi wa umeme wa solar katika kituo cha
Buhangija.Alisema lengo la CSI ni kusaidia shughuli za kuendeleza
elimu,michezo,kuboresha afya na kutunza mazingira kwa watoto wenye
ulemavu mbalimbali wakie wa ngozi na wasioona,wasiosikia na wenye
ulemavu mbalimbali,tunaamini ulemavu siyo kikwazo kwa watoto kufikia
malengo yao ya kimasomo na kimaisha
Tunafuatilia kinachoendelea hapa...
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika kituo
cha Buhangija ambapo mbali na kupongeza jitihada za Miss Tanzania mwaka
2012 kufanikisha kupatikana kwa huduma ya umeme katika kituo hicho
aliwaomba wadau wengine kufika katika kituo hicho kwani matatizo ya
kituo hicho hayawezi kumalizwa na serikali pekee
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza jambo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alitumia fursa hiyo
kuwakemea watu wote wanaowinda watu wenye albinism na kuongeza kuwa
serikali haitasita kuwachukulia hatua kali wakibainika
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza jambo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiendelea kuzungumza
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akipanda mti wa kumbukumbu katika kituo cha Buhangija
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na Rais na Mwanzilishi wa
Brigitte Alfred Foundation bi Brigitte Alfred wakipanda mti
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na Rais na Mwanzilishi wa
Brigitte Alfred Foundation bi Brigitte Alfred wakimwagilia maji mti
walioupanda
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza jambo baada ya kupanda mti
Msimamizi wa Kituo cha Buhangija Seleman Kipanya na mratibu wa Brigitte Alfred Foundation Stanley Mosha wakipanda mti
Watoto wakicheza muziki mbele ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Mwanzilishi wa Brigitte Alfred Foundation Brigitte Alfred akicheza muziki na watoto
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifungua michezo kwa watoto,walimu na walezi wa watoto katika kituo cha Buhangija
Tunasubiri kuona michezo ya watoto,walimu na walezi wa watoto..
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiteta jambo na Rais na Mwanzilishi wa Brigitte Alfred Foundation Brigitte Alfred
Rais na Mwanzilishi wa Brigitte Alfred Foundation Brigitte Alfred akiangalia shindano la kuchora
Kushoto ni mwakilishi wa Kampuni ya wakandarasi wa umeme -CSI Electrical
Limited Joan Kahwa,Rais na Mwanzilishi wa Brigitte Alfred Foundation
Brigitte Alfred na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
wakishuhudia jinsi watoto wanavyochora vitu mbalimbali
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akachukua kalamu kwa ajili ya kuchora
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro naye akaamua kuanza kuchora
Shindano la mbio za magunia likaendelea
Watoto katika kituo cha Buhangija
Mchezo wa kuvuta kamba ukiendelea kati ya walimu na walezi wa watoto katika kituo cha Buhangija likiendelea
Katika shindano hilo walezi wa watoto (kushoto) waliibuka washindi
Mratibu wa taasisi ya Brigitte Foundation bwana Stanley Mosha akieleza
jinsi taasisi yao inavyojali watoto katika maeneo mbalimbali nchini
Tanzania ikiwemo kituo cha Kabanga mkoani Kigoma
Rais na Mwanzilishi wa Brigitte Alfred Foundation bi Brigitte Alfred (wa pili kushoto) akifurahia jambo
Mwenyekiti wa ALAT taifa na mstahiki meya wa manispaa ya
Shinyanga,mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam akizungumza katika kituo cha
Buhangija ambapo aliipongeza taasisi ya Brigitte Alfred Foundation kwa
kujali watoto ambapo wamejenga bweni na kufanikisha kufungwa kwa umeme
wa solar
Mwenyekiti wa ALAT taifa na mstahiki meya wa manispaa ya
Shinyanga,mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam alitumia fursa hiyo kuwaomba
wadau mbalimbali kuendelea kuwasaidia watoto hao kwani ni dhawabu kubwa
kusaidia watoto hao wenye mahitaji maalum
Mwenyekiti wa ALAT taifa na mstahiki meya wa manispaa ya
Shinyanga,mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam aliyekuwa ameambatana na
mwenyekiti wa wapanda baiskeli Shinyanga bwana Tungu Johnson (wa pili
kushoto) aliwapongeza pia Waendesha baiskeli katika manispaa ya
Shinyanga kuona umuhimu wa kutoa msaada wa chakula ikiwemo maharage kilo
40,mchele kilo 80,unga wa sembe kilo 85,mafuta ya kupikia lita 10 na
tenga la nyanya vyote vikiwa na thamani ya shilingi 300,000/- kwa ajili
ya watoto hao
Muda wa chakula ukawadia- Watoto
wakiwa katika foleni kwa ajili ya chakula kilichoandaliwa na taasisi ya
Brigitte Alfred Foundation na CSI Electrical Limited (picha zipo hapo
chini).
Chakula na vinywaji vikiwa tayari kwa ajili ya watoto wenye
albinism,wasioona na wasiosikia katika kituo cha Buhangija katika
manispaa ya Shinyanga
Watoto wakichukua chakula
Watoto wakiendelea kula chakula
Watoto wenye ulemavu wa kutoona wakichukua chakula
Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred akimlisha chakula mmoja wa watoto katika kituo cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga
Zoezi la kula likiendelea
Kushoto ni mwakilishi wa Kampuni ya wakandarasi wa umeme -CSI Electrical
Limited Joan Kahwa akimpa soda mtoto mwenye albinism katika kituo cha
Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.
Post a Comment