0

Bi Hillary Clinton anayegombea kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha Democratic, amemchagua aliyekuwa wakati mmoja Seneta wa jimbo la Virginia Tim Kaine, kama mgombea mwenza katika Uchaguzi wa Novemba mwaka huu.
Bi Clinton amemweleaea Tim Kaine kama mtu aliyejitolea maisha yake yote kupigania haki za wengine.
Akifurahia uteuzi huo Seneta Kaine mwenyewe amesema ametunukiwa kupe hadhi hiyo ya kuchaguliwa na kuwa yuko tayari kuanza kampeni mara moja.
Waandishi wa habari wanasema kuwa aneheshimiwa sana kama mtu anaetegemewa sana , anayeweza kuwavutia wapiga kura wasio fungamana na vyama vya kisiasa Marekani na hata Wanachama wa Republican wenye msimamo wa kadri.
Hata hivyo wanachama wengine wa Democratic wanamdhania kuwa mtu asiye na mawazo huru kwa kiwango wanavyotaka wao.
Bi Clinton na Senetor Kaine watateuliwa rasmi kama wogombezi wa Democratic katika Mkutano wa Baraza Kuu la chama hicho , utakaoanza Jumatatu.

Post a Comment

 
Top